Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Zanzibar yarejea kibabe

ZPL Pict

Muktasari:

Kwenye Uwanja wa Mao B kisiwani Unguja, KMKM itacheza dhidi ya Uhamiaji ambapo mara ya mwisho kukutana msimu uliopita, KMKM ilishinda kwa mabao 2-0. Uhamiaji inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi ya kupoteza mechi tatu mfululizo za ZPL msimu huu, hivyo itahitaji kushinda ili kufikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya tatu kutoka ya nne iliyopo sasa.

LIGI Kuu ya Zanzibar (ZPL) imerejea baada kupisha michuano ya Kombe la FA ambapo sasa ni mzunguko wa tisa ambapo jana baada ya kuchezwa mechi mbili kati ya Raskazone dhidi ya Wembe huku Muembe Makumbi ikichuana na Chipukizi, leo Alhamisi kuna mitanange mingine miwili.

Kwenye Uwanja wa Mao B kisiwani Unguja, KMKM itacheza dhidi ya Uhamiaji ambapo mara ya mwisho kukutana msimu uliopita, KMKM ilishinda kwa mabao 2-0. Uhamiaji inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi ya kupoteza mechi tatu mfululizo za ZPL msimu huu, hivyo itahitaji kushinda ili kufikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya tatu kutoka ya nne iliyopo sasa.

KMKM nayo haipo pazuri, pointi zake kumi zinaiweka nafasi ya nane, hivyo suala la ushindi linahitaji pande zote mbili ili kujiweka pazuri kwenye msimamo.

Pia kuna Mlandege dhidi ya Zimamoto, zitachuana kwenye Uwanja wa Mao A kisiwani Unguja, huku ikikumbukwa kwamba timu hizo zilipokutana mara ya mwisho Mlandege iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Zimamoto ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 19, ikifunga mabao 11 na kufungwa matano, Mlandege inakamata nafasi ya nane ikiwa na pointi 11. Timu hizo zikikutana zinakuwa na ushindani kubwa kutokana na ukongwe na historia nzuri ilizonazo kwenye Ligi Kuu Zanzibar.

Kibarua kingine kipo kwa Fufuni iliyokuwa haijashinda mechi hata moja kati ya nane ilizocheza, itaikaribisha JKU, Novemba Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, huku mchezo wa mwisho Fufuni ikipokea kipigo cha mabao 2-1.

Siku hiyo ya Novemba 1, 2026, pia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ waliopo nafasi ya tatu, watachuana na Mafunzo kwenye Uwanja wa Mao A, huku Mafunzo ikiwa na historia ya kufungwa mabao 3-1 mechi ya mwisho walipokutana. Mafunzo haikuanza vizuri msimu huu, hadi sasa imeshinda mechi moja pekee kati ya nane ilizocheza, ipo nafasi ya 14 ikikusanya pointi saba.

Raundi hii ya tisa, itashuhudiwa mechi mbili zinazokutanisha timu kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Zanzibar ambazo zitapigwa Jumamosi Oktoba 31, 2026, Black Sailors itacheza dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Mao B, na Mwenge dhidi ya Kipanga kwenye Uwanja wa Gombani.