Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chasambi mambo safi Kagera Sugar

Muktasari:

  • Chasambi mwenye umri wa miaka 22, alianza kujijenga katika soka la ushindani akiwa Mtibwa Sugar kabla ya kujiunga na Simba Januari 2024, ambako alikutana na ushindani mkubwa wa kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

KAGERA Sugar imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Ladack Chasambi kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja, ikiwapiku Namungo FC na Geita Gold zilizokuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania huduma ya mchezaji huyo baada ya kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars.

Chasambi mwenye umri wa miaka 22, alianza kujijenga katika soka la ushindani akiwa Mtibwa Sugar kabla ya kujiunga na Simba Januari 2024, ambako alikutana na ushindani mkubwa wa kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Baada ya kujiunga na Simba, alicheza mechi tatu za ligi katika msimu wa 2023/24 na kufunga mabao matatu. Msimu wa 2024/25 alicheza mechi tatu na kufunga bao moja, huku msimu wa 2025/26 akicheza mechi tatu bila kufunga.

Msimu huu alijiunga na Singida Black Stars akitokea Simba, lakini hakupata nafasi kubwa ya kucheza kabla ya kuvunja mkataba na kuwa mchezaji huru. Usajili huo unakuja wakati Kagera ikihitaji kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji, hasa baada ya kurejea Ligi Kuu Bara msimu huu na kutaka kujihakikishia nafasi nzuri kwenye msimamo.

Taarifa za ndani zilieleza kuwa Kagera imeamua kuingia kwa nguvu katika mazungumzo na mchezaji huyo baada ya kubaini kuwa anaweza kuongeza kasi, ubunifu na ushindani katika eneo la pembeni ya ushambuliaji.

“Chasambi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Kagera na ataanza kazi rasmi dirisha dogo msimu huu, lengo ni lile lile kuhakikisha kwamba, kikosi kinakuwa na nguvu kubwa eneo la mbele.”

Hatua hiyo imezikatisha tamaa Namungo na Geita Gold ambazo zilikuwa zikimfuatilia kwa karibu, kila moja ikiwa na sababu zake za kumhitaji.

Namungo ilikuwa imeingia kwenye vita hiyo kupitia kocha wake Juma Mgunda, ambaye aliwahi kufanya kazi na Chasambi alipokuwa Simba na anaufahamu vizuri uwezo wa mchezaji huyo.

Kurejea kwake Kagera ni nafasi nyingine ya kuanza upya na kujenga rekodi mpya, huku akihitaji kuthibitisha kwamba bado ana uwezo wa kuwa miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa katika ligi.