Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Humwambii kitu Shekhan na namba 10

Muktasari:

  • Msimu huu wa 2026/27, Shekhan ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Yanga ameanza kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake akiwa Singida, ambako amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika michezo kadhaa, huku akiweka rekodi ya kufunga mabao mawili mpaka sasa ya Ligi Kuu, huku akifunga moja kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

UWEZO wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani ni moja ya silaha zinazomfanya Shekhan Ibrahim Khamis kuwa mchezaji mwenye manufaa kwa Singida Black Stars msimu huu, lakini pamoja na kuwa na uwezo wa kucheza kuanzia kiungo mkabaji hadi winga ya kulia, kiungo huyo ana nafasi moja anayoipenda kuliko nyingine zote, nayo ni namba 10.

Msimu huu wa 2026/27, Shekhan ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Yanga ameanza kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake akiwa Singida, ambako amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika michezo kadhaa, huku akiweka rekodi ya kufunga mabao mawili mpaka sasa ya Ligi Kuu, huku akifunga moja kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumzia uwezo huo, Shekhan alisema anaweza kucheza nafasi hizo kulingana na mahitaji ya timu, lakini namba 10 ndiyo anayojisikia vizuri zaidi anapokuwa uwanjani.

“Ninaweza kucheza nafasi za mbele kuanzia namba sita, namba nane, namba 10 ndiyo namba yangu, na winga ya kulia. Namba tisa siwezi kucheza,” alisema kiungo huyo.

Safari ya Shekhan haikuanza Yanga wala Singida, bali katika akademi ya JKU Visiwani Zanzibar aliyojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 11. Baadaye alipitia Zanzibar Combine kabla ya kupata nafasi ya kujiunga na Yanga Desemba 2023, akiwa na umri wa miaka 18.

Jangwani alianza katika kikosi cha pili kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa. Msimu wa 2023/24 alicheza mechi saba za Ligi Kuu, huku msimu wa 2025/26 akicheza mechi nane na kufunga bao moja. Baadaye alihamia Singida Black Stars kwa mkopo ili kupata nafasi kubwa zaidi ya kucheza na kuendeleza kipaji chake.

Pamoja na kuondoka Yanga, bado anaendelea kupata ushauri kutoka kwa baadhi ya wachezaji aliocheza nao, akiwamo Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya, ambao humpongeza anapofanya vizuri na kumwelekeza maeneo anayohitaji kuboresha.