Mkenya kupambania hili Chama la Wana
Muktasari:
- Kocha huyo aliyezifundisha timu mbalimbali za Tanzania zikiwemo za Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, amejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2025-2026.
KOCHA Mkuu wa Stand United, ‘Chama la Wana’, Mkenya Yusuf Chippo amesema moja ya kazi kubwa aliyokuwa nayo katika kikosi hicho ni kutengeneza balansi nzuri ya maeneo mawili muhimu ya safu yote ya ushambuliaji na kwenye eneo pia la kujilinda.
Kocha huyo aliyezifundisha timu mbalimbali za Tanzania zikiwemo za Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, amejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2025-2026.
Chippo amesema licha ya mwenendo mzuri wa kikosi hicho hadi sasa, ila bado hakuna muunganiko mzuri wa safu ya ushambuliaji sawa na ile ya kujilinda, jambo linalochangia kutokuwa na balansi bora ya mabao msimu huu.
“Katika mechi zetu tano tumefunga mabao matano na kuruhusu pia matano, maana yake hatuna balansi nzuri wakati tunafunga na tukishambuliwa, tunahitaji kuifanyia kazi kwa haraka ili kutengeneza uwiano mzuri wa maeneo yote,” amesema Chippo.