Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chippo aibukia Chama la Wana

CHIPPO Pict

Muktasari:

  • Jukumu kubwa la kocha huyo ni kuipambania Stand United kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu wa 2018-2019, ikiwa nafasi ya 19 na pointi 44, baada ya kushinda mechi 12, sare nane na kupoteza 18, huku ikifunga mabao 38 na kuruhusu 50.

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mkenya Yusuf Chippo amefikia makubaliano ya kujiunga na kikosi cha Stand United 'Chama la Wana' ya mjini, Shinyanga, kwa lengo la kuipambania katika Ligi ya Championship kwa msimu huu wa 2026-2027.

Kocha huyo aliyezifundisha timu mbalimbali za Tanzania zikiwemo za Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United zamani Tabora United, amejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chippo amesema amewasili Tanzania kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu huu wa 2026-2027, huku kwa sasa baadhi ya taratibu zikiendelea kukamilishwa na uongozi wa kikosi hicho uliomrejesha nchini.

"Ni kweli nipo Tanzania kwa ajili ya kujiunga na Stand United, makubaliano ya awali ni ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha, malengo ni ya kuipambania ipande daraja kutoka Ligi ya Championship hadi Ligi Kuu Bara," amesema Chippo.

Chippo alijiunga na Mtibwa Sugar, Novemba 17, 2025, akitokea Murang'a SEAL ya Kenya msimu wa 2025-2026, timu hiyo ilishuka daraja hadi Championship, iliposhika nafasi ya 15 na pointi 27, ikishinda mechi sita, sare tisa na kupoteza 15.

Kocha huyo anakumbukwa na mashabiki hasa baada ya kukiongoza kikosi cha Ulinzi Stars kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Kenya 'KPL' kati ya 2003 na 2005 na kuhudumu akiwa kocha msaidizi wa Harambee Stars kuanzia 2008 hadi 2011.

Jukumu kubwa la kocha huyo ni kuipambania Stand United kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu wa 2018-2019, ikiwa nafasi ya 19 na pointi 44, baada ya kushinda mechi 12, sare nane na kupoteza 18, huku ikifunga mabao 38 na kuruhusu 50.