Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mtanzania: Ligi ya Ukraine imenikomaza

BEKI Pict

Muktasari:

  • Pia beki huyo alicheza katika mashindano yaliyopita ya kufuzu AFCON yaliyofanyika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam mwaka 2024 na alitoa mchango mkubwa uliowezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa ukanda wa CECAFA.

BEKI wa kushoto wa timu ya vijana ya Polissya Zhytomyr U19 ya Ukraine, Ismail Ally Omar amesema kitendo cha kucheza soka la kulipwa nchini humo kimemsaidia kukua na kukomaa kiakili kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi hiyo ya Ulaya.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17, aliyeanzia soka lake katika akademi ya Azam FC, amesema ligi ya Ukraine ni miongoni mwa ligi ngumu na ili mchezaji apate nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza inamlazimu kufanya vitu vya ziada na kujituma zaidi ya wenzake anapokuwa mazoezini.

Akizungumza na Mwanaspoti beki huyo amesema kwake kupata nafasi katika kikosi hicho ni jambo zuri linalompa furaha, pia linamwongezea chachu ya kuendelea kupambana kwa sababu anatambua ndio kwanza anaanza safari yake ya soka la ushindani katika ngazi ya kimataifa.

"Kucheza ligi ya Ukraine kumenikomaza sana kiakili kwani ni ligi yenye ushindani wa hali ya juu na si rahisi kupata nafasi kama huna kitu cha ziada. Hii inanipa chachu ya kupambana zaidi kwa sababu bado niko mwanzoni mwa karia yangu," amesema beki huyo.

Mchezaji huyo anayetumia mguu wa kushoto na anayeweza kucheza pia kama kiungo wa kushoto, ameeleza mafanikio ya mtanzania mwenzake, Novatus Miroshi (Dismas) alipokuwa akiitumikia Shakhtar Donetsk ya Ukraine, yamefungua milango na kufanya wachezaji wa Kitanzania waaminiwe zaidi nchini humo.

Mbali na klabu, Ismail ana uzoefu mkubwa wa kimataifa na alikuwa sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kilichoshiriki mashindano ya kufuzu AFCON U-20 mwaka huu na Tanzania iliondolewa kwa penalti 4-3 na Sudan katika fainali baada ya kutoka sare ya 1-1.

Pia beki huyo alicheza katika mashindano yaliyopita ya kufuzu AFCON yaliyofanyika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam mwaka 2024 na alitoa mchango mkubwa uliowezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa ukanda wa CECAFA.