Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikakati mipya ya Wembe

WEMBE Pict

Muktasari:

  • Wembe ilishuka dimbani dhidi ya Raskazone katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao A, Unguja, ambapo timu hizo zilitoka 0-0.

KOCHA wa Wembe, Ally Manyani, amesema timu yake imejipanga kuhakikisha inakusanya pointi tatu katika kila mchezo, huku ikiwa tayari kukubali pointi moja pale ushindi unaposhindikana, ikiwemo katika michezo ya ugenini.

Wembe ilishuka dimbani dhidi ya Raskazone katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao A, Unguja, ambapo timu hizo zilitoka 0-0.

Manyani amesema kupata pointi moja katika mchezo huo si matokeo mabaya kwa timu yake, akizingatia maandalizi waliyofanya kabla ya mchezo huo.

Ameongeza kuwa kikosi chake kina matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo ujao, huku benchi la ufundi likipanga kurekebisha makosa yaliyojitokeza.

Kocha huyo amesema wachezaji wake wote wako salama na wanaendelea kujiandaa kwa michezo inayofuata ili kuongeza nafasi ya timu hiyo kupata matokeo mazuri.

“Malengo yetu ni kukusanya pointi mapema ili kujihakikishia nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. Ndiyo maana tumejipanga kupambana katika michezo yetu miwili ya ugenini,” amesema Manyani.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Raskazone, Salum Ali Haji, amesema timu yake haikubahatika kupata ushindi licha ya kujiandaa vizuri kwa mchezo huo.

Amesema walitarajia kupata pointi zote tatu kutokana na maandalizi waliyofanya, lakini akakiri kuwa pointi moja waliyopata nayo ni muhimu katika safari yao ya ligi.