Mido yashusha presha Songea United
Muktasari:
- Katika mechi nne ilizocheza timu hiyo kabla ya jana Jumapili dhidi ya Kigamboni United, imetoka sare tatu na kupoteza moja, ikiwa nafasi ya 11 na pointi tatu, huku safu ya ushambuliaji ikifunga bao moja na kuruhusu mawili.
KIUNGO wa Songea United, Gilbert Boniface amesema licha ya kikosi hicho kupitia kipindi kigumu cha kukosa ushindi hadi sasa msimu huu, ila bado wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi, kutokana na aina ya wachezaji bora na wazoefu walionao.
Akizungumza na Mwanaspoti, Boniface amesema sababu ya mwenendo wa timu hiyo umechangiwa na kuchelewa kuanza maandalizi ya msimu (Pre Season), ingawa kadri wanavyozidi kucheza wanazidi kujipata taratibu, jambo linaloongeza morali kikosini.
“Katika mechi nne tulizocheza tumepoteza moja na kutoka sare tatu, sio mwenendo mbaya kutokana na ushindani uliopo, ila tunahitaji kupambana zaidi ili tutakapofika hadi raundi 15, za kwanza tuwe kwenye nafasi nne za juu,” amesema Boniface.
Kiungo huyo mshambuliaji amesema uwepo wa wachezaji wapya wengi katika kikosi hicho ni sababu nyingine ya kutofanya vizuri, ingawa wanaendelea kutengeneza muunganiko wa uchezaji.
Katika mechi nne ilizocheza timu hiyo kabla ya jana Jumapili dhidi ya Kigamboni United, imetoka sare tatu na kupoteza moja, ikiwa nafasi ya 11 na pointi tatu, huku safu ya ushambuliaji ikifunga bao moja na kuruhusu mawili.