Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mido Fountain Gate yaongeza mzuka

Muktasari:

  • Kiungo huyo alipata jeraha la goti ambalo lilimuweka nje kwa miezi sita katika mechi ya timu hiyo dhidi ya Mashujaa FC, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na kuisha sare ya kufungana bao 1-1, Machi 13, 2026.

BAADA ya kukosekana kwa kipindi cha miezi sita, kiungo wa Fountain Gate, Daniel Joram ameanza mazoezi rasmi na kikosi hicho, jambo lililomuibua kocha mkuu wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’ anayefurahia kurejea tena kwa mchezaji huyo.

Kiungo huyo alipata jeraha la goti ambalo lilimuweka nje kwa miezi sita katika mechi ya timu hiyo dhidi ya Mashujaa FC, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na kuisha sare ya kufungana bao 1-1, Machi 13, 2026.

Katika mechi hiyo ambayo ni ya msimu wa 2025-2026, wenyeji Mashujaa walipata bao la utangulizi kupitia Juma Nyenyezi dakika ya 55, kisha Fountain Gate ikachomoa dakika ya 90+3, lililofungwa na Sadick Ramadhan.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya urejeo wa nyota huyo, Minziro alisema ni habari nzuri kwa mchezaji mwenyewe na benchi la ufundi kiujumla, kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

“Ni habari njema kwake kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake, ila hata kwetu benchi la ufundi kwa sababu uwepo wake ni muhimu na unatuongezea wigo wa machaguo kikosini kutokana na ufinyu wa wachezaji tulionao kwa sasa,” alisema Minziro.

Minziro alisema kuanza mazoezi kwa kiungo huyo na wachezaji wenzake ni jambo nzuri na hadi kufikia Oktoba 7, 2026, kabla ya kurejea kwa mechi za Ligi Kuu Bara, atakuwa yupo fiti zaidi kwa asilimia 100, kuanza kucheza ndani ya kikosi hicho.

Joram alijiunga na Fountain Gate Desemba 27, 2024, akitokea Pamba Jiji, ingawa baada ya mkataba wake wa mkopo wa miezi sita kuisha na kikosi hicho cha Mwanza, Juni 30, 2025, alisajiliwa moja kwa moja na kusaini mkataba wa miaka miwili.