Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jayrutty, Mangungu wapitishwa na BMT

NGUNGU Pict

Muktasari:

  • Katika nafasi ya Urais, majina matatu yamepitishwa ambayo ni Stephen Mosha, Joseph Rwegasira 'Jayrutty' na Issa Mangungu. Jina moja halijapitishwa ambalo ni Wasiwasi Mwabulambo.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Ijumaa, Novemba 20, 2026 limetangaza orodha ya watia nia waliopitishwa na walioenguliwa kugombea nafasi tofauti za uongozi wa Kamisheni ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC)

Katika nafasi ya Urais, majina matatu yamepitishwa ambayo ni Stephen Mosha, Joseph Rwegasira 'Jayrutty' na Issa Mangungu. Jina moja halijapitishwa ambalo ni Wasiwasi Mwabulambo.

Katika nafasi ya Makamy wa Rais, jina moja limepitishwa ambalo ni Frderick Lori huku Jacob Mbuya akienguliwa. Mtia nia pekee wa nafasi ya Uwakilishi Wanawake, Christinah Koroso amepitishwa kuwania nafasi hiyo.

Kanda nne zina mgombea mmoja mmoja aliyepitishwa ambazo ni Kaskazini, Kati, Ziwa na Magharibi. Wagombea hao ni Rosemary Massawe wa Kanda ya Kaskazini, Dk. Anicetus Lusale (Kanda ya Kati), Chase Masanja (Kanda ya Ziwa) na Hashir Masangula (Kanda ya Magharibi).

Kanda ya Mashariki ina wagombea wawili waliopitishwa ambao ni Bakari Khatibu na Abdallah Mtulamesu. Uchaguzi Mkuu wa Kamisheni ya Kusimamia ngumi za kulipwa (TPBRC) umepangwa kufanyika Novemba 24, 2026.