Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi za ufunguzi Ligi Kuu Bara, Kagere awapa raha Simba

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 unaanza leo Jumatano kwa timu mbalimbali kushuka uwanjani kuanza kazi ya kuinyang’anya Simba ubingwa.

Viwanja sita vitawaka moto ambapo Simba watawakaribisha Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Ligi hiyo ilizinduliwa na mechi ya Simba na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mechi ya Ngao ya Jamii.

Hata hivyo, ligi hiyo inaanza ikiwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa wadhamini.

LIVE KUTOKA

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

TFF yafanya mabadiliko mechi ya Simba yasogezwa saa 2 usiku badala ya saa moja kama ilivyotangwaza jana na uongzo wa Simba

Simba vs Prisons  (Saa 2:00 usiku)

Mashabiki wanaendelea kuingia uwanjani

Muda wowote mechi itaanza

Dakika ya pili shuti kali la Kagere linatinga nyavuni.
Ilikuwa pasi ya Kichuya ambayo ilimkuta Bocco ambaye aliweka pasi ya kisigino kwa Kagere ambaye alifunga bao hilo.

Meddie Kagere anaipatia Simba bao la kuongoza dakika ya 2'

Dakika ya 18 na 19, Simba wanafanya mashambulizi mawili langoni mwa Prisons kupitia kwa Shiza Kichuya na Hassan Dilunga lakini mabeki wa Prisons wanakuwa makini kuokoa hatari hizo

Dakika ya 30' Simba 1-0 Prisons

Dakika ya 34, kipa wa Prisons, Aron Kalambo anaumiabaada ya kugongana na Hassan Dilunga wakati alipokua kwenye harakati za kuokoa shambulizi la Simba. Baada ya kutibiwa kwa dakika tatu, anarejea uwanjani kuendelea na mchezo

TAHMINI  DAKIKA 45 KIPINDI CHA  KWANZA NA MCHAMBUZI THOBIAS SEBASTIAN

DAKIKA 45 kipindi cha kwanza Timu zinakwenda mapumziko. Simba ikiongoza bao 1-0

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika kwa Simba wakiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Kagere dakika ya 2.

Simba walionekana kuimarika zaidi na kutawala mpira na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia.

Kichuya ambaye alikuwa akicheza kama kiungo wa pembeni amekuwa mwiba kwa Prison kwani ndio mpishi wa nafasi hizo.

Kama Simba wangekuwa makini wangeweza kufunga bao zaidi ya moja ambalo walifunga kwani Kagere, Bocco, Kichuya na Dilunga walikosa nafasi za wazi.
 
Prison ambao walimaliza kipindi cha kwanza bila ya makali yoyote kwa kushindwa kutengeneza nafasi ya kufunga.

Dakika ya 64 Prisons wanaoneka kuwa fiti kwenye pumzi

Uwanja wa Kaitaba,  Kagera

Kagera Sugar vs Mwadui  (Saa 10 jioni)

Mechi inaendelea...

Mwadui FC ipo mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar

 Bao la Mwadui limefungwa dakika ya 9 na Salum Ije

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Omary Mponda (20, 29)

Dakika 45 timu zinakwenda mapumziko Kagera Sugar  2-1 Mwadui

FT: Kagera Sugar 2- 1 Mwadui

Uwanja wa Mabatini, Pwani

Ruvu Shooting vs Ndanda FC (Saa 10 jioni)

Mechi inaendelea...

Mawingu yametanda Malandizi kiashirilia cha mvua kunyesha lakini jua nalo linachomoza kwa mbali.

Dakika 45 Ruvu Shooting 0-0 Ndanda.

Dakika ya 68 Vitalis Mayanga ameiandikia Ndanda FC. Ruvu Shooting 0-1 Ndanda

FT: Ruvu Shooting 0-1 Ndanda

Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza

Alliance FC vs Mbao FC  (Saa 10 jioni)

Wakati homa ya pambano la 'Mwanza Darby' kati ya Alliance na Mbao ikiendelea kupamba moto jijini hapa rekodi zinaonyesha Alliance kufa mapema katika mchezo huo wa kwanza kwenye Ligi Kuu inayotarajia kupigwa leo Jumatano saa 10:00 jioni kwenye dimba la Kirumba. (Mwandishi Saddam Sadick)

KIKOSI CHA ALLIANCE HIKI HAPA

1/ Kelvin- Richard 18
2/ Israel- Patrick 03
3/ Hance- Masoud 06 (C)
4/Wema- Sadock 25
5/Geofley- Luseke 15
6/ Joseph- Majagi 02
7/Shabani- William 04
8/ Mapinduzi- Barama 07
9/ Chinedu- Michael 19
10/ David- Richard 20
11/ Juma- Nyangi 12

AKIBA

1/ Said- Lubawa 01
2/Godlove- Mdumule 05
3/Rajabu- Kibera 23
4/Martin- Kigg 21
5/Dickson- Ambundo 17
6/Nchembe- Maganda 14
7/Wayyeka - Tatuwe 29

Vikosi vya Mbao FC na Alliance FC vinapasha na muda wowote mechi inaanza

Mechi inaendelea...

Dk ya 10 Hamim Abdul anapiga shuti kali linagonga besela na kutoka nje,Mbao wanalisakama lango la Alliance

Dakika ya 13' Alliance 0-0 Mbao FC

Dakika ya 22 mabao 0-0

Dk ya 26 Hamim Abdul wa Mbao anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu David Richard

Mbao wanakosa bao dakika ya 28'

Alliance FC inakwenda mapumziko matokeo yakiwa 0-0 dhidi ya Mbao FC

Dk ya 79 Evaligestus Mujwahuki anaipatia bao la kwanza Mbao kwa krosi safi kutoka wingi ya kulia

FT: Alliance 0-1 Mbao FC

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

Coastal Union vs Lipuli FC    (Saa 10 jioni)

Mchezo unaendelea....

Dakika ya 40' Coastal Union 0-0 Lipuli

Zimeongezwa dakika 2 kipindi cha kwanza

Dakika 45 kipindi cha kwanza Coastal Union 0-0 Lipuli

Lipuli wanapata bao kupitia kwa Zawadi Mauya dakika ya 58. Coastal Union 0-1 Lipuli

Coastal Union wanasawazisha bao dakika ya 69. Coastal Union 1-1 Lipuli bao likifunga na Bakari Mnyeto

FT: Coastal Union 1-1 Lipuli

Uwanja wa Namfua, Singida

Singida United vs Biashara United (Saa 10 jioni)

Mechi inaendelea....

Dakika ya 18 Biashara United inapata bao la kwanza kupitia kwa George Wiliam

Dakika ya tano Singida wamepata kona

Mapro wa Singida wasugua benchi kutokana na madai ya kutokuwa na vibali vya kazi

Kutoka Uwanja wa Namfua, mechi haina mwamuzi msaidizi wa kwanza na mpira ni mapumziko Biashara United ikiongoza bao 1-0

Singida United na Biashara mpira unaendelea ikiwa ni dakika za majeruhi na muda wowote mpira utamalizika