Laizer bado hakijaeleweka Gunners FC
Muktasari:
- Timu hiyo inashiriki Ligi ya Championship kwa msimu wa pili sasa tangu ilipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza msimu wa 2025-2026 na kumaliza ikiwa nafasi ya nane na pointi 38, baada ya kushinda mechi 11, ikitoka sare tano na kupoteza 14.
KOCHA Mkuu wa Gunners FC ya jijini, Dodoma, Mohamed Ismail 'Laizer', amesema mwenendo wa timu hiyo sio mzuri sana wala mbaya hadi sasa katika mechi ilizocheza, ingawa wanapaswa kuongeza nguvu ili kuendana na ushindani mkubwa unaoendelea.
Akizungumza na Mwanaspoti, Laizer amesema timu hiyo inakabiliwa na mambo mawili muhimu ya kufanyia kazi kwa haraka ili kuendana na ushindani na moja ni kuboresha safu bora ya kujilinda, sawa na ushambuliaji kwa lengo la kuongeza kasi.
"Bado hatuko sehemu salama zaidi kwa sababu ushindani kwa sasa ni mkubwa hasa kwa mechi za ugenini, tunahitaji kuongeza kasi na ili tufanikishe hilo, ni lazima tuhakikishe tuna safu bora ya kujilinda na ile ya ushambuliaji," amesema Laizer.
Laizer amejiunga na Gunners FC baada ya kukaa kwa muda bila kufundisha timu yoyote, tangu mara ya mwisho alipoachana na Fountain Gate inayocheza Ligi Kuu, Aprili 10, 2026, akichukua nafasi ya Henry Mkanwa aliyeifundisha msimu wa 2025-2026.
Gunners FC inayoshiriki Ligi ya Championship kwa msimu wa pili tangu ipande daraja msimu wa 2024-2025, imeshinda mechi moja tu, sare tano na kupoteza mbili, ikishika nafasi ya 10 na pointi nane, huku ikifunga mabao sita na kuruhusu saba.
Timu hiyo inashiriki Ligi ya Championship kwa msimu wa pili sasa tangu ilipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza msimu wa 2025-2026 na kumaliza ikiwa nafasi ya nane na pointi 38, baada ya kushinda mechi 11, ikitoka sare tano na kupoteza 14.