Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi 3 tu, Yanga yachana mkataba wa Maxi

MASHABIKI wa Yanga kuna jina jipya wamempa kiungo wao mshambuliaji Maxi Nzengeli wakimuita ‘Discipline Master’ yaani mwalimu wa nidhamu lakini mabosi wao nao, wameanza na hesabu mpya baada ya kuchana mikataba ya awali ya baadhi ya nyota na kuwapa mingine.

Jina hilo jipya alilopewa Nzengeli ni ile vaa yake nadhifu akiwa uwanjani akichomekea muda wote hata mazoezini huku kiwango chake kikiwa cha juu baada ya kutumika kwenye michezo mitatu ambayo mashabiki wameiona.

Nzengeli licha ya kucheza muda mrefu eneo la kiungo, lakini hadi sasa hajaonyeshwa kadi yoyote zaidi ya kuupiga mwingi akiwateka mashabiki wa Yanga na hata wale wa upinzani kwa pasi zake murua ndefu kwa fupi.

Mabosi wa Yanga sasa wako kwenye hatua za mwisho kumboreshea mkataba wake, ikiwa ni pamoja na kumpa gari la kisasa atakalokuwa anatanua nalo mjini, jambo ambalo halikuwepo kwenye mkataba wa awali aliokubaliana nao.

Hesabu hizo hazitakuwa kwa Nzengeli pekee, pia beki wao wa kulia Kouassi Yao ambaye amekuwa kwenye kiwango kikubwa, wawili hao wakithibitisha ubora wao ndani ya muda mfupi kwenye kikosi hicho ambacho msimu huu kitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Wachezaji bora wameonekana na bado wako wengi tutawaboreshea masilahi yao, hawa wawili haraka kwa upande wa malipo yao tumeshaanza kuyaboresha na hata kuwapa magari ya kutembelea ikiwa ni kitu kipya kwenye mikataba yao,”alisema bosi huyo wa juu.

“Hii ni muendelezo wetu kwa kuthamini kazi nzuri ya wachezaji wetu wanayoifanya uwanjani, pia ni chachu kwa wengine nao kujituma kama wenzao na wao wakionyesha kazi nzuri viongozi na hata mashabiki wataona, hawa nafikiri hakuna mwenye swali nao.

Tangu watue Yanga msimu huu Nzengeli na Yao wamekuwa wachezaji muhimu wakiwavutia mashabiki wa timu hiyo kwa kazi yao bora ndani ya uwanja.

Wamefanikiwa kuonyesha ubora wao kwenye mchezo wa kwanza wa Kilele cha Siku ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, wakakipiga mchezo wa Ngao dhidi ya Azam na mchezo wao wa mwisho kucheza ni dhidi ya Simba fainali ya Ngao Jumapili iliyopita, mchezo ambao Yanga walipoteza kwa penalti 3-1.

Wakati huohuo, kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema pamoja na kushindwa kutetea taji la Ngao ya Jamii kikosi chake kipo imara na kinauchu wa kushindana huku asikisitiza kazi iliyopo ni kusuka safu ya ushambuliaji.

“Hatupaswi kuweka kichwani matokeo mabaya ambayo tuliyapata, hasira zote tunazielekeza kimataifa na Ligi Kuu, tunaanza na Asas FC tunahitaji matokeo mazuri kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea hatua inayofuata.

“Wachezaji walicheza vizuri na wapo kwenye mazingira mazuri ya kushindana sina wasiwasi na wao kwenye hilo matokeo yaliyotokea ni sehemu ya mchezo na penati hazina mwenyewe.” alisema.