Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mcongo wa Geita aanza tambo

Muktasari:

  • Nyota huyo amefikia makubaliano ya kutoongeza mkataba mpya na waajiri wake wa zamani wa Namungo FC, baada ya kukitumikia kikosi hicho cha ‘Wauaji wa Kusini’ kwa misimu mitatu, tangu alipojiunga nayo kwa mara ya kwanza kwa msimu wa 2023-2024.

BAADA ya Geita Gold kuinasa saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Namungo FC, ‘Wauaji wa Kusini’, Mkongomani Fabrice Ngoy, nyota huyo ameweka wazi anataka kuendelea kufanya vizuri na kikosi hicho, licha ya ushindani mkubwa wa kuwania nafasi.

Nyota huyo amefikia makubaliano ya kutoongeza mkataba mpya na waajiri wake wa zamani wa Namungo FC, baada ya kukitumikia kikosi hicho cha ‘Wauaji wa Kusini’ kwa misimu mitatu, tangu alipojiunga nayo kwa mara ya kwanza kwa msimu wa 2023-2024.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ngoy alisema baada ya kuachana na Namungo kuna timu mbalimbali alizofanya nazo mazungumzo kwa ajili ya kuzichezea, ingawa ofa ya Geita Gold ilikuwa ni nzuri na ndipo akaamua kujiunga nayo ili kuendeleza ubora wake. “Wakati nipo nyumbani DR Congo nilifuatwa na klabu mbalimbali ila siku tatu zilizopita Geita Gold ilinitumia mkataba na baada ya kuusoma nikaona ni mzuri kisha nikasaini miaka miwili, lengo langu ni kuendelea kufanya vizuri,” alisema Ngoy.

Ngoy alijiunga na Namungo msimu wa 2023-2024, akitoka Kitayosce iliyobadilishwa jina na kuitwa Tabora United na sasa TRA United, baada ya kuifungia mabao 15 ikiwa Ligi ya Championship, nyuma ya kinara, Edward Songo wa JKT Tanzania aliyefunga 18.

Mshambuliaji huyo alitua hapa nchini kwa mara ya kwanza msimu wa 2022-2023, akitokea Real Nakonde FC ya Zambia na msimu wa 2023-2024, alifunga bao moja tu la Ligi Kuu Bara, huku 2024-2025, akifunga mawili na msimu wa 2025-2026, alifunga 11.

Ngoy anaenda kuungana na washambuliaji wengine ndani ya kikosi hicho wakiwemo, Mzambia Obrey Chirwa aliyetamba na timu za Yanga, Azam FC, Namungo FC, Kagera Sugar na KenGold, huku akianza vizuri baada ya kufunga bao moja la Ligi Kuu Bara.

Chirwa aliyejiunga na Geita Gold baada ya kuachana na Kagera Sugar, ameanza vyema maisha yake na kikosi hicho, baada ya kuifungia pia bao muhimu la Ligi Kuu Bara, katika ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0, dhidi ya Mbeya City, Agosti 14, 2026.

Nyota huyo alikuwa ni mfungaji bora wa Ligi ya Championship msimu wa 2025-2026, akiwa na Kagera Sugar baada ya kufunga mabao 18, sawa na Maulid Shaban wa Geita Gold ambaye wameungana naye tena kucheza timu moja, huku akiongezeka pia Ngoy.