Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khaleed Aucho atua Ethiopia

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyeitumikia Singida kwa msimu mmoja tangu ajiunge nayo Agosti 16, 2025, akitokea Yanga, ameiwezesha kutwaa taji la Kombe la Kagame mwaka 2025, kisha kucheza pia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.

ALIYEKUWA kiungo wa Singida Black Stars, Mganda Khalid Aucho amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Sidama Bunna FC ya Ethiopia, baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Kenya Police FC na AFC Leopards zote za Kenya zilizomuhitaji awali.

Nyota huyo aliyeitumikia Singida kwa msimu mmoja tangu ajiunge nayo Agosti 16, 2025, akitokea Yanga, ameiwezesha kutwaa taji la Kombe la Kagame mwaka 2025, kisha kucheza pia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.

Kiungo huyo aliyejiunga na Yanga, Agosti 9, 2021, akitokea Misr Lel Makkasa SC ya Misri, alikuwa muhimili mkubwa wa timu hiyo na kutwaa mataji tofauti, ikiwemo Ligi Kuu, Ngao ya Jamii, Kombe la CRDB, Kombe la Muungano na Kombe la Mapinduzi.

Kwa kipindi cha miaka minne aliyocheza Yanga, Aucho amejitengenezea umaarufu mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji kwa ufasaha, jambo ambalo tangu aondoke ndani ya kikosi hicho, mabosi wa timu hiyo wamesumbuka sana kupata mbadala wake.

Licha ya kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, ila nyota huyo ameondoka Singida akiwa ameifungia bao moja la Ligi Kuu Bara alilolifunga msimu wa 2025-2026, katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 4-1, dhidi ya kikosi cha Mbeya City, Mei 26, 2026.

Nyota huyo amefikia uamuzi wa kuondoka Singida baada ya kushindwa kufikia makubaliano mapya ya kuongeza mkataba mpya, huku klabu mbalimbali zikionyesha kumuhitaji kutokana na uzoefu wake, kabla ya Sidama Bunna FC ya Ethiopia kumsajili.

Kiungo huyo amewahi kucheza timu mbalimbali zikiwemo za Tusker FC, Gor Mahia FC za Kenya, Baroka FC (Afrika Kusini), FK Crvena zvezda, OFK Beograd zote kutokea Serbia, East Bengal FC na Churchill Brothers FC za India kwa mafanikio makubwa.