Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchora katuni Mwananchi King Kinya afariki dunia

MCHORAJI Pict

Muktasari:

  • Kinya alihudumu kama mchora katuni katika magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya MCL

MFANYAKAZI wa Idara ya Habari ya kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Kinyagulo Tuzo maarufu kama King Kinya, amefariki dunia leo, Septemba 17, 2026 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Taarifa iliyotolewa Ofisi ya Rasilimali watu MCL imethibitisha kutokea kifo cha  King Kinya aliyehudumu kwa miaka 17 kama mchora katuni wa magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kaka wa marehemu, Kiondo Tuzo Mjema, amesema King Kinya alianza kuugua akiwa nyumbani Tabata mwanzoni mwa Julai 2026, hali iliyomfanya kukaa ndani kwa muda kabla ya kupelekwa Morogoro.

Amesema akiwa Morogoro hali yake ilizidi kuwa mbaya na baadaye alipelekwa hospitalini, ambako alilazwa kwa takribani wiki moja kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani.

“Alipotoka hospitali aliambiwa arudi tena kwa ajili ya ufuatiliaji. Juzi alirudi hospitalini baada ya kusumbuliwa na tumbo, kuharisha na kutapika, akapewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani,” amesema.

Kwa mujibu wa Kiondo, hali ya marehemu ilizidi kuwa mbaya usiku wa kuamkia jana Septemba 15, 2026, akilalamikia maumivu makali ya tumbo na kichwa pamoja na kutapika na kuharisha.

Kiondo amesema msiba upo Kimara Kona  na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Mwananyamala.