Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhamiaji FC vinara wa Ligi Kuu Zanzibar

Muktasari:

  • Uhamiaji FC ilijipatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza likifungwa kwa kichwa na Abel Simwinga dakika ya 31 kufuatia kona safi iliyochongwa na Seif Samgela.

KLABU ya Uhamiaji, imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar baada ya jana Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fufuni FC, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

Uhamiaji FC ilijipatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza likifungwa kwa kichwa na Abel Simwinga dakika ya 31 kufuatia kona safi iliyochongwa na Seif Samgela.

Kipindi Cha pili, timu zilirejea kiwanjani kwa kuanza kushambuliana kwa zamu, ndipo Uhamiaji FC ikapata bao la pili dakika 52 likitiwa kimiani na mshambuliaji Yahya Haji Karoa baada ya kupokea mpira wa adhabu uliopigwa na Ali Juma Maarifa "Mabata".

Katika mchezo huo, Uhamiaji FC imevunja rekodi ya kutopata alama sita kwenye Kisiwa cha Pemba tangu timu hiyo ipande Ligi Kuu Zanzibar misimu minne iliyopita. Awali walipata ushindi wa 2-0 dhidi Mwenge FC kwenye mchezo uliopita.

Ushindi huu, unaiweka Uhamiaji FC kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 12 baada ya kushinda michezo yote minne iliyocheza msimu huu.

Uhamiaji FC itashuka tena dimbani Septemba 24, 2026 kwa kucheza na Raskazone FC kwenye Uwanja wa Mao kisiwani Unguja.

Matokeo mengine ya mechi za jana Jumatano katika Ligi Kuu Zanzibar ni Polisi 1-1 Zimamoto na Mwenge 1-2 Black Sailors.