Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchawi wa Simba ni kasi, morali

Mchawi wa Simba ni kasi, morali

Muktasari:

Simba itarudiana na Platnum kati ya Januari 5 na 6 mwakani kwenye Uwanja wa Mkapa.

Dar es Salaam. Simba inaihitaji kuongeza umakini na kasi ya ufungaji kama inahitaji kushinda mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ya Zimbambe.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walikubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika juzi mjini Harare na ina kazi ya kufanya kushinda zaidi ya bao moja katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kati ya Januari 5 na 6 jijini, ili kutinga hatua ya makundi.

Kwa siku za karibuni, kasi ya ufungaji wa mabao katika kikosi hicho imeonekana kupungua tofauti na walipoanza ligi.

Katika mechi tano za mashindano yote yakiwemo ya kimataifa, Simba imefunga mabao manne, jambo ambalo linaweza kuwaweka katika wakati mgumu kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Platinum.

Katika mchezo wa juzi dhidi ya FC Platinum, Simba ilionekana kutokuwa na ushirikiano katika ukabaji pindi timu hiyo ilipokosa mpira, jambo lililosababisha mabeki wa timu hiyo kupata wakati mgumu kuwazuia Platnum, hasa mfungaji, Perfect Chikwende, Kutsanzira Rahman, Gift Mbwete, waliokuwa na kasi ya ajabu.

Pia kasi ambayo Platinum waliionyesha katika mchezo huo ilionekana kuwazidi wachezaji wengi wa Simba ambao walishindwa kuhimili.

Mchawi wa Simba ni kasi, morali

Beki wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ alisema washambuliaji wa Simba wanatakiwa kuchangamka kwani bado wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo marudiano .

“Ukiangalia mechi ya jana (juzi) Simba waliathiriwa na kasi ya wapinzani wao, lakini kama wangekuwa wamechangamka hada kule mbele basi wangeimaliza ile mechi huko huko ugenini,” alisema Malima.

Kocha Mrage Kabange alisema Simba wanatakiwa wasijiamini kupita kiasi katika mechezo wa marudiano bali wacheze kwa tahadhari na waongeze umakini eneo la ushambuliaji ili waweze kupata mabao.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck alisema: “Hatukustahili kupoteza mchezo. Tulitawala mechi muda mwingi wa mchezo na tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga ila hatukuwa bora katika eneo hilo ingawa tulikuwa kupata hata sare.”

Mchawi wa Simba ni kasi, morali

Simba inawasili nchini leo na kujiandaa na mchezo wao ujao wa Kombe la FA dhidi ya Majimaji, Jumapili.