Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbongo apandishwa timu ya wakubwa Ufaransa

SHIL 01

Muktasari:

  • Soann, ambaye anacheza nafasi ya kiungo, sasa ameandaliwa kuingia katika mazingira ya timu ya wakubwa, hatua ambayo inaweza kuwa sehemu muhimu kwake kuelekea kikosi cha kwanza cha Grenoble kinachoshiriki Ligue 2.

KIUNGO Mbongo, Soann Shabani amepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Grenoble Foot 38 ya Ufaransa baada ya kuaminika na benchi la ufundi kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwenye mfumo wa vijana wa klabu hiyo.

Soann, ambaye anacheza nafasi ya kiungo, sasa ameandaliwa kuingia katika mazingira ya timu ya wakubwa, hatua ambayo inaweza kuwa sehemu muhimu kwake kuelekea kikosi cha kwanza cha Grenoble kinachoshiriki Ligue 2.

Kilichofanya apandishwe ni kiwango bora alichoonyesha pamoja na mchango mkubwa alioutoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana U-17 Serengeti Boys, ambako alikuwa sehemu ya kikosi kilichoiwakilisha Tanzania katika AFCON U17 Morocco 2026.

Kocha wa timu hiyo, Franck Rizzetto amesema Soann kama ataendelea kuonyesha uwezo wake basi anaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho.

"Ni kweli tumekuwa na kawaida ya kupandisha vijana wale tunaowaona wameanza kupata uzoefu nafikiri Soann anaweza kuongeza kitu kwenye eneo la kiungo na naamini kwa jinsi tulivyofanya naye mazoezi alichoonyesha anaweza kuwa kiungo tegemeo wa baadae," amesema kocha huyo raia wa Ufaransa.

Soann alikuwa miongoni mwa vijana waliopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwenye mashindano hayo, huku Serengeti Boys ikiandika historia ya kucheza fainali ya AFCON U17 kwa mara ya kwanza.

Tanzania ilifika hatua hiyo baada ya kuiondoa Misri kwa penalti katika nusu fainali. Katika fainali iliyochezwa Rabat, Serengeti Boys ilitoa ushindani mkubwa dhidi ya Senegal na kulazimisha sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90, kabla ya Senegal kushinda kwa penalti 4-2 na kutwaa ubingwa. Matokeo hayo yaliifanya Tanzania kumaliza nafasi ya pili katika mashindano hayo ya Afrika na kufuzu kucheza Kombe la Dunia la vijana.

Kinda huyo aliyezaliwa mwaka 2009 nchini humo mama yake raia wa Ufaransa huku baba yake akiwa Mtanzania, kabla ya kuitumikia Grenoble Foot 38 aliichezea St Etienne Academy ya vijana chini ya miaka 15.