Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Mtanzania anakiwasha Sweden

SHILLA Pict
SHILLA Pict

Muktasari:

  • Shilla, mwenye miaka 18, amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaovutia zaidi katika ligi ya vijana ya Allsvenskan U19, akicheza nafasi za ushambuliaji.

KINDA wa Tanzania, Mohammed Shilla ameanza vizuri kwenye akademi ya AIK ya Sweden baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza mabao katika msimu wa 2025/2026 akitokea Azam FC.

Shilla, mwenye miaka 18, amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaovutia zaidi katika ligi ya vijana ya Allsvenskan U19, akicheza nafasi za ushambuliaji.

Katika michezo 10 aliyocheza msimu huu, Shilla ametengeneza rekodi ya kufunga mabao 12 na kutoa asisti tano, akichangia idadi ya mabao 17. Amecheza jumla ya dakika 804, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa wachezaji wenye tija kubwa kwenye mashindano hayo.

SHIL 02

Takwimu hizo zimemweka Shilla katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi ya Allsvenskan U19. Kwa wastani huo wa uzalishaji mabao.

Kabla ya kuhamia Sweden, Shilla alikuwa sehemu ya mfumo wa vijana wa Azam FC, moja ya akademi zinazotajwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuzalisha vipaji Tanzania.

Uwezo wake wa kufunga, kutengeneza nafasi na kufanya maamuzi sahihi akiwa karibu na lango umekuwa sehemu ya mafanikio yake msimu huu.

SHIL 03

Kama ataendelea na kasi hiyo, macho ya mashabiki wa soka Tanzania yataendelea kuwa kwake, huku safari yake kutoka Azam FC hadi AIK ikiwa mfano mwingine wa namna akademi za Matajiri wa Chamazi zinavyoweza kuwa daraja la vipaji.