Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbilinyi, Kidedea kila mtu atamani kumtoa nungu mwenzake

MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Vicent Mbilinyi na Saidi Mpoma ‘Kidedea’  wamesaini mkataba wa kucheza katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika Septemba 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo mabondia hao walitamba kila mmoja akidai atashinda pambano hilo na kuwaomba mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kumuunga mkono.
Bondia Mbilinyi alisema kuwa ameanza maandalizi kwa ajili ya pambano hilo kwa nia ya kutaka kushinda, kwa kuwa ngumi kwake ni ajira ataiheshimu sana ajira hiyo na kamwe hatafanya utani katika kazi yake.
Aidha mratibu wa pambano hilo Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema kuwa kutakuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi siku hiyo, Fred Sayuni atacheza na Haidari Mchango wakati George Dimoso atazipiga na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’.
Pambano jingine litawakutanisha Imani Mapambano dhidi ya Paul Kamata, Sadiki Momba atacheza na Mohamed Kashinde, huku Tonny Rashidi akimkabili Said Zungu  na Ramadhani Shauri atapanda ulingoni kuzichapa na Saidi Amani.
Super D alisema ili kutowachosha mashabiki watakaoingia ukumbini siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali ya muziki. (Mwandishi Wetu).