Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele, Kapombe kwenye vita yao CAF

Muktasari:

  • Hata hivyo wawili hao sasa wamejikuta wakikutanishwa lakini nje ya uwanja baada ya wote kuteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Klabu za Afrika wa mwaka 2025.

Fiston Mayele na Shomari Kapombe hawajakutana uwanjani tangu Mayele alipojiunga na Pyramids FC ya Misri mwaka 2023 akitokea Yanga.

Hata hivyo wawili hao sasa wamejikuta wakikutanishwa lakini nje ya uwanja baada ya wote kuteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Klabu za Afrika wa mwaka 2025.

Katika orodha iliyotolewa na CAF leo ya wachezaji 10 wanaowania tuzo hiyo, Mayele na Kapombe wametajwa.

Mchango ambao wawili hao wameutoa kwa klabu zao katika msimu uliopita umeonekana kuwabeba na kuwafanya waingie katika kinyang’anyiro hicho.

Mayele aliiongoza Pyramids FC kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ambapo aliifungia mabao sita yaliyomfanya awe Mfungaji Bora.

Kapombe alitoa mchango mkubwa kuiwezesha Simba kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akicheza zaidi ya asilimia 90 ya mechi zote.

Ukiondoa Mayele na Kapombe, nyota wengine wanaowania tuzo hiyo ni Ismail Belkacem, Blati Toure, Issoufou Dayo, Emam Ashour, Ibrahim Adel, Mohamed Hrimat, Mohamed Chibi na Oussama Lamlioui.