Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matengenezo ya barabara yastopisha magari kuingia Uhuru

Muktasari:

  • Tofauti na dabi nyingine zilizopita ambapo magari yalikuwa yanaruhusiwa kupita eneo hilo na kupaki, kutokana na ujenzi huo ni maroli yanayomwaga michanga na yale yanayochimba vifusi.

MATENGENEZO yanayoendelea katika barabara ya Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, yamefanya magari kupaki mbali kidogo na uwanjani.

Tofauti na dabi nyingine zilizopita ambapo magari yalikuwa yanaruhusiwa kupita eneo hilo na kupaki, kutokana na ujenzi huo ni maroli yanayomwaga michanga na yale yanayochimba vifusi.

Kutoka uwanja wa Uhuru hadi chuo cha  Duce, hakuna magari yanayopita hata daladala, kwani kuna maeneo yana vifusi na ujenzi unaendelea.

Mbali na hilo hali ya shamrashamra na hamasa siyo kubwa hadi sasa,huenda hali hiyo ikabadilika kadri muda unavyokwenda.

Kuna magari mengine yanazuiwa barabarani, isipokuwa yenye vibali maalumu ndiyo yanaruhusiwa kupita, ingawa pia linapita gari moja moja.

Leo saa 1:00 usiku itapigwa dabi ya Kariakoo ambapo Simba itakuwa mwenyeji ikiikaribisha Yanga.

Msimu uliyopita wa 2025/26  mzunguko wa kwanza ambayo Yanga ilikuwa mwenyeji wa Simba, mechi hiyo ilipigwa  Uwanja wa New Amaan, Zanzibar timu hizo zilitoka suluhu, wakati iliyopigwa Jenerali Isamuhyo zilitoka sare ya mabao 2-2.