Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye jina la Messi Bongo wafunguka

Muktasari:

  • Messi amestaafu  kuichezea  Argentina baada ya kuitumikia miaka 21, amefunga mabao 126 katika mechi 208 alizocheza, tofauti na mastaa hapa nchini waliyopachikwa jina lake, wengi wao wametoka nje ya ramani ya soka mapema.

KUSTAAFU kwa supastaa wa soka duniani Lionel Messi, katika timu ya taifa ya Argentina kumewaibua mastaa nchini, waliowahi kulitumia jina lake la pili  kama a.k.a zao.

Messi amestaafu  kuichezea  Argentina baada ya kuitumikia miaka 21, amefunga mabao 126 katika mechi 208 alizocheza, tofauti na mastaa hapa nchini waliyopachikwa jina lake, wengi wao wametoka nje ya ramani ya soka mapema.

Katika mahojiano ya Mwanaspoti na baadhi ya wachezaji hao, wengi wao walianza kumfuatilia anachokifanya Messi uwanjani baada ya kuanza kuitwa jina hilo,  kabla ya hapo walikuwa wanawafuatilia wachezaji wengine.


RAMADHAN SINGANO

Nyota wa zamani wa Simba Azam TP Mazembe na Taifa Stars Ramadhan Singano, anasema mtu wa kwanza kumwita jina la Messi ni kocha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi Selemani Matola, ambapo  kila alipokuwa akifanya mazoezi alikuwa analitaja jina hilo kwa kumfananisha na baadhi ya vitu alivyokuwa anavifanya staa huyo zikiwemo chenga.

"Kocha Matola alivyokuwa ananiita jina hilo mara kwa mara, ingawa sikuwahi kutarajia mashabiki watalifikisha mbali, nilijua lingeishia mazoezini, ndiyo nilikuwa sivimbi na jina hilo zaidi  kufanya kazi yangu, lakini binafsi sikuwahi kujifananisha na Messi kwani najua ni mchezaji mkubwa na kipaji cha aina yake" anasema Singano na kuongeza:

"Sikuwahi kuwa shabiki wa Messi wala Ronaldo, isipokuwa nilikuwa napenda ushindani wao uwanjani, ambao ndiyo umeibua utimu duniani kote wengine wakijiita timu Ronaldo wengine timu Messi hilo limekuja baada ya wao kuonyesha uwezo mkubwa katika mpira wa miguu ila binafsi naangalia mchezaji ambaye anafanya vizuri ila sina upande baina ya hao mastaa."


ISSA ABUSHEE 'MESSI'

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Issa Abushee anasema alianza kuitwa jina la Messi akiwa na timu ya mtaani ya Stone Barg ya Kariakoo na mtu aliyempachika a.k.a hilo anamtaja kwa jina la Ulembe Sela.

"Nakumbuka nilikuwa Madrasa alikuja huyo kaka Sela kumuomba Ustadhi ili nikamfanyie dua nyumbani kwake, lakini lengo lake alitaka niende kuisaidia timu yao kucheza mechi ya kirafiki nakumbuka tulichezea Uwanja wa Villa Squad, wakati nipo uwanjani akaanza kuniita Messi tangu hapo likawa jina ninaloitwa mtaani" anasema na kuongeza:

"Wakati nasajiliwa Coastal Union msimu wa 2017/18 kama U-20 kocha Juma Mgunda, alikuwa amepewa taarifa zangu kwamba naitwa Messi baada ya kuonana naye tu akawa ananiita Messi badala ya kwenda kucheza kikosi B, aliwaambia viongozi huyo atacheza timu kubwa katika kikosi hicho nilikutana na kaka yangu anaitwa Raizin Hafidh nilikuwa nimecheza naye Bom Bom FC yeye pia ndiye aliyefanya jina hilo liwe kubwa zaidi."

Kabla ya kuitwa jina hilo anasema alikuwa shabiki wa Didier Drogba lakini baada ya kuona jina la Messi linakuwa kubwa alianza kumfuatilia uchezaji wake."Kwanza changamoto ilikuwa ni ukubwa wa huyo mtu nililazimika kujituma kwa bidii angalau niwe nafanya vitu vya maana uwanjani, sijawahi kufikia viatu vyake ila kwa sehemu kuna baadhi ya vitu nilikuwa naviiga kutoka kwake ila ingekuwa amri yangu nilipenda niitwe jina langu zaidi."


ABDALLAH MGUHI

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Abdallah Mguhi alianza kuichezea kikosi B, baadaye akapandishwa timu ya wakubwa kutokana na uwezo wake uwanjani wa kupiga chenga wakawa wanamuita Messi wa Yanga ingawa umaarufu wa jina hilo haukudumu kwa muda mrefu.


IBRAHIM TWAHA

Mchezaji wa zamani wa Simba na Coastal Union Ibrahim Twaha:"Jina la Messi nilianza kuitwa nikiwa Coastal hata baada ya kujiunga na Simba nikashangaa bado mashabiki wananiita jina hilo, ndipo nikaanza kumfuatilia Messi anachofanya uwanjani kabla ya hapo sikuwa namfuatilia ingawa baada ya kuanza kumfuatilia nikawa naiga baadhi ya vitu.

Anaongeza: "Kiukweli sijafikia kile ambacho amefanya Messi ni kipaji adimu ndiyo maana dunia inawashindanisha Ronaldo na Messi kulingana na mafanikio ya hali ya juu na legasi waliyoijenga katika mpira wa miguu."