Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mko wapi? Uhuru ni kweupe

Muktasari:

  • Kwa kawaida, mchezo wa Simba na Yanga huambatana na shamrashamra za mashabiki wanaowasili mapema, wakiwa wamevalia jezi za timu zao, huku nyimbo, vifijo na mijadala ya hapa na pale vikitawala mazingira ya uwanja.

ZIMESALIA saa chache kabla ya Simba na Yanga kukutana kwenye Dabi ya Kariakoo, lakini hali ya Uwanja wa Uhuru ni tofauti na ilivyozoeleka siku za dabi, huku mashabiki waliofika wakionekana kuwa wachache na uwanja ukiwa bado mweupe.

Kwa kawaida, mchezo wa Simba na Yanga huambatana na shamrashamra za mashabiki wanaowasili mapema, wakiwa wamevalia jezi za timu zao, huku nyimbo, vifijo na mijadala ya hapa na pale vikitawala mazingira ya uwanja.

Hata hivyo, safari hii hali ni tofauti kwani uwanja haujaonesha pilika pilika zilizotarajiwa katika mchezo mkubwa kama huu, hali inayofanya mazingira ya kabla ya dabi kukosa msisimko uliozoeleka.

Mashabiki wa timu hizo mbili wamezoea kuifanya siku ya dabi kuwa ya kipekee, kuanzia mitaani hadi viwanjani, lakini kwa sasa hali ya Uwanja wa Uhuru haioneshi picha hiyo ya ushindani na hamasa.

Simba na Yanga zinatarajiwa kushuka dimbani saa 1:00 jioni, katika pambano linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini.

Kwa mashabiki wa soka, huu sio mchezo wa kawaida, bali ni nafasi ya kuonesha mapenzi kwa timu zao na kujivunia ushindi dhidi ya watani hao wa jadi.

Hata hivyo, kwa hali ilivyo sasa, Uwanja wa Uhuru bado ni kweupe, tofauti na hamasa kubwa ambayo mashabiki wameizoea kila Simba na Yanga zinapokutana.