Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa watia neno kwa Barker, Manqoba

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Aliyekuwa kocha wa Azam FC, Mashujaa na Tanzania Prisons Meja Mstaafu Abdul Mingange amesema:”Makocha wa timu hizo ni wazuri wa mbinu hivyo mechi itakuwa ya kiufundi na mbinu zaidi ngumu kusema mapema kwamba Simba au Yanga itashinda ila ninachokitarajia ni mechi ya ushindani na isiyo na mabao mengi.”

KARIAKOO dabi inayotarajiwa kupigwa Oktoba 10, Simba ikiwa mwenyeji dhidi ya Yanga imechambuliwa na mastaa wa zamani wa timu hizo jinsi itakavyokuwa ngumu na ushindani wa mbinu wa makocha Steve Barker na Manqoba Mngqith wote wakiwa raia wa Afrika Kusini.

Mwanaspoti lilizungumza na mastaa hao kwa nyakati tofauti jambo kubwa zaidi wamechambua ubora wa klabu hizo ulioonekana miaka ya hivi karibuni namna utakavyofanya mechi iwe bora na ngumu.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Malimi Busungu amesema: “Simba imekuwa na mabadiliko makubwa ya pafomasi natarajia itakuwa mechi ngumu na dakika 90 ndizo zitakazoamua nani ataibuka na pointi tatu eneo ninaloona litakuwa na bato kali ni viungo.

Ameongeza:” Simba kuna Clatous Chama (mabao manne)Libasse Gueye(asisti tano) kwa Yanga kuna Maxi Nzengeli (mabao matatu)Mudathir Yahya (mabao mawili) na wengine wachezaji hao wanafanya vizuri jambo lingine mbinu za makocha kocha wa Yanga anaonekana anapenda kushambulia zaidi na kocha wa Simba inategemeana kuna mechi anaacha iwe wazi zingine anashambulia na kuzuia.”

Kwa upande wa staa wa zamani wa Simba Meddie Kagere, amesema kwa uzoefu wake mechi ya dabi inakuwa na sapraizi za kushangaza:”Kwanza wachezaji morali zinakuwa juu naamini itakuwa ni mechi nzuri yenye ushindani kwani timu zote zina wachezaji wazuri.”

Staa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Sekilojo Chambua amesema:”Yanga ina kikosi kipana ni kocha namna atakavyokipanga kulingana na ushindani wa mechi ya dabi Simba kuna Gueye na Oura wana nguvu mikimbio mizuri na umiliki wa mpira miguuni hao wanaweza wakawa mwiba kwa Yanga.”

Aliyekuwa kocha wa Azam FC, Mashujaa na Tanzania Prisons Meja Mstaafu Abdul Mingange amesema:”Makocha wa timu hizo ni wazuri wa mbinu hivyo mechi itakuwa ya kiufundi na mbinu zaidi ngumu kusema mapema kwamba Simba au Yanga itashinda ila ninachokitarajia ni mechi ya ushindani na isiyo na mabao mengi.”