Mastaa tisa wampasua kichwa Ibenge
Muktasari:
- Juzi kocha wa timu ya Taifa Taifa Stars, Miguel Gamondi aliita kikosi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 huku Azam ikiwa na wachezaji wengi zaidi kuliko timu nyingine zote, baada ya mastaa tisa wa timu hiyo kuitwa kati ya wachezaji 42.
KOCHA wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema anafurahia kuona wachezaji wake tisa wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, lakini amekiri hatua hiyo imemuweka kwenye changamoto kubwa katika maandalizi ya kikosi chake.
Juzi kocha wa timu ya Taifa Taifa Stars, Miguel Gamondi aliita kikosi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 huku Azam ikiwa na wachezaji wengi zaidi kuliko timu nyingine zote, baada ya mastaa tisa wa timu hiyo kuitwa kati ya wachezaji 42.
Akizungumza na Mwanaspoti Ibenge alisema wachezaji hao ni sehemu muhimu ya mipango yake, hivyo kuondoka kwao kwenda kwenye majukumu ya Taifa kunapunguza muda aliokuwa ameupanga kuutumia wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa za FIFA katika kujenga muunganiko wa kikosi chake.
Mastaa wa Azam walioitwa ni Zuberi Foba, Aishi Manula, Lameck Lawi, Twalib Nuru, Pascal Msindo, Himid Mao, Feisal Salum, Abdulkarim Kiswanya na Abdul Suleiman.
Alisema kuwa, kipindi hicho kilikuwa muhimu kwake baada ya muda wa maandalizi ya msimu mpya kutokuwa wa kutosha katika kambi ya maandalizi ya msimu ‘pre-season’.
Alisema sasa atalazimika kutumia mbinu nyingine kuhakikisha anawafanyia maboresho wachezaji watakaobaki kambini, huku akisubiri kurejea kwa wale watakaokuwa kwenye majukumu ya Taifa.
“Ninafurahia kuona wachezaji wangu tisa wameitwa Taifa Stars kwa sababu hii ni heshima kwao na kwa klabu. Lakini kwa upande mwingine, hii ni changamoto kwetu kwa sababu tulitaka kutumia kipindi hiki cha mapumziko kujenga muunganiko wa timu,” alisema Ibenge.
Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji hao tisa ni muhimu katika mfumo anaotaka kuutumia msimu huu, hivyo kutokuwepo kwao kunamlazimisha kutafuta njia mpya za kuhakikisha muda uliopo hautapotea.
Kikosi kamili:
MAKIPA
1. Zuberi Foba — Azam FC
2. Aishi Manula — Azam FC
3. Yona Amos — Singida Black Stars
4. Metacha Mnata — Singida Black Stars
5. Hussein Masalanga — Young Africans
MABEKI
6. Ibrahim Bacca — Young Africans
7. Bakari Mwamnyeto — Young Africans
8. Lameck Lawi — Azam FC
9. Twalib Nuru — Azam FC
10. Vedastus Masinde — Simba SC
11. Mohammed Mussa — Young Africans
12. Danillo Maino — FK Panevezys, Lithuania
13. Haji Mnoga — Patro Eisden, Ubelgiji
14. Bakari Msimu — Simba SC
15. Nickson Kibabage — Simba SC
16. Mohammed Hussein — Young Africans
17. Anthony Mlugo — Simba SC
18. Pascal Msindo — Azam FC
19. Nathaniel Chilambo — Simba SC
VIUNGO
20. Novatus Miroshi — Göztepe, Uturuki
21. Himid Mao — Azam FC
22. Adolph Mtasigwa — Kaizer Chiefs, Afrika Kusini
23. Yusuf Kagoma — Simba SC
24. Mohamed Sagaf — Eastbourne Borough, Uingereza
25. Alphonse Mabula — JS Kabylie, Algeria
26. Charles Mmombwa — Zabbar, Malta
27. Mudathir Yahya — Young Africans
28. Feisal Salum — Azam FC
29. Sheikhan Khamis — Singida Black Stars
30. Morice Abraham — Simba SC
31. Abdulkarim Kiswanya — Azam FC
WASHAMBULIAJI
32. Tarryn Allarakhia — Boreham Wood, Uingereza
33. Simon Msuva — Newroz, Iraq
34. Bernard Kamungo — FC Dallas, Marekani
35. Kelvin John — Aalborg, Denmark
36. Kibu Denis — Al Nasr, Libya
37. Abdul Suleiman — Azam FC
38. Sabri Kondo — Häcken, Sweden
39. Cyprian Kachwele — HFX Wanderers, Canada
40. Said Khamis — Hajafungamana na timu
41. Selemani Mwalimu — Young Africans
42. Paul Peter — JKT Tanzania