Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dube anafanya balaa huko

Muktasari:

  • Nyota huyo amejiunga na Hardrock FC ya kwao Zimbabwe na tayari msimu huu wa 2026-2027, ameonyesha kiwango kizuri, baada ya kuhusika na mabao saba, kufuatia kufunga manne na kuasisti matatu katika mechi sita alizozicheza kikosini humo.

ALIYEKUWA mshambuliaji nyota wa Yanga, Prince Dube ameendeleza kiwango bora katika Ligi Kuu ya Zimbabwe akiwa na kikosi cha Hardrock FC, tangu alipoachana na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026, rasmi, Julai 2, 2026.

Nyota huyo amejiunga na Hardrock FC ya kwao Zimbabwe na tayari msimu huu wa 2026-2027, ameonyesha kiwango kizuri, baada ya kuhusika na mabao saba, kufuatia kufunga manne na kuasisti matatu katika mechi sita alizozicheza kikosini humo.

Kiwango hicho kimemfanya mshambuliaji huyo kuchaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Zimbabwe mwezi uliopita.

Dube aliyeachana na Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026, alikuwa na ofa mbalimbali kutoka katika klabu mbalimbali, ingawa alichagua kujiunga na Hardrock FC ya kwao Zimbabwe akiamini ni sehemu nzuri kwake.

Nyota huyo alijiunga na Yanga, Julai 6, 2024, akitokea Azam FC na kutwaa mataji mbalimbali, ikiwemo Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, akiwa ni mshambuliaji tegemeo kwa kikosi hicho, alichoamua kuachana nacho na kujiunga na Hardrock FC.

Katika misimu yake miwili aliyoichezea Yanga, nyota huyo alihusika kwenye mabao 37 ya Ligi Kuu Bara, baada ya msimu wa kwanza wa 2024-2025, kufunga 13 na kuasisti manane, huku msimu uliopita wa 2025-2026, akifunga 10 na kuasisti sita tu.

Msimu bora kwa Dube katika Ligi Kuu Bara ni wa 2020-2021 alipojiunga na Azam FC kwa mara ya kwanza akitokea Klabu ya Highlanders ya kwao Zimbabwe ambapo nyota huyo alionyesha kiwango bora na kumaliza nafasi ya tatu kwa wafungaji bora.

Kwa msimu huo wa 2020-2021, mshambuliaji huyo aliifungia Azam FC mabao 14 ya Ligi Kuu Bara, akizidiwa na washambuliaji wenzake nyota Chris Mugalu aliyekuwa na 15 na mfungaji bora msimu huo John Bocco aliyefunga 16 wote wakicheza Simba.