Mastaa sita KMC pancha

KMC FC inakabiliwa na changamoto ya wachezaji sita tegemeo  ambao ni majeruhi  ndani ya kikosi hicho ambapo kwasasa wanaendelea na matibabu,kwa mujibu wa Ofisa Habari, Christina Mwagala.
Wachezaji hao ni Hance Masound ambaye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big stars. Wengine ni Ibrahim Ame, Baraka Majogoro ambao pia kwa nyakati tofauti katika mchezo huo uliomalizika kwa KMC FC kupoteza kwa bao moja ugenini walishindwa kuendelea na mchezo kutokana na kupata majeraha.
Wengine ni Kelvin Kijili, Awesu Ally Awesu pamoja na Emmanuel Mvuyekure ambao hawa pia walikuwa na majeraha ya muda mrefu.
KMC FC itaanza mazoezi leo kujiandaa na mechi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Novemba 28 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.