Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maskauti Hispania watua Dar Youth

MASKAUTI Pict

Muktasari:

  • Ugeni huo kutoka Ulaya unalenga kuwafungulia milango ya fursa za kimataifa wachezaji wanaoshiriki michuano hiyo ya msimu wa saba na maskauti hao tayari walishuhudia mechi ya Kundi B kati ya Bulls Football Academy dhidi ya Brothers Jr na kuonyesha kuvutiwa sana na viwango vya baadhi ya wachezaji.

MASHINDANO ya soka ya vijana ya Dar Youth Cup U-18 yameingia katika sura mpya baada ya ujio wa wawakilishi kutoka akademia mashuhuri ya Spain Rush-SPF ya Hispania, waliowasili nchini kutazama na kusaka vipaji vya wachezaji chipukizi.

Ugeni huo kutoka Ulaya unalenga kuwafungulia milango ya fursa za kimataifa wachezaji wanaoshiriki michuano hiyo ya msimu wa saba na maskauti hao tayari walishuhudia mechi ya Kundi B kati ya Bulls Football Academy dhidi ya Brothers Jr na kuonyesha kuvutiwa sana na viwango vya baadhi ya wachezaji.

Spain Rush-SPF ambayo ina makao yake makuu jijini Valencia, imekuwa ikishirikiana na klabu mbalimbali za Hispania ambazo zimekuwa zikiwapelekea wachezaji waliolelewa katika akademi hiyo.

Michuano ya Dar Youth Cup ilianza wikiendi iliyopita huku timu za  TDS na Bulls Football Academy zikianza kwa kishindo kwa ushindi mnono walioupata katika mechi zao za ufunguzi zilizopigwa kwenye viwanja vya Ufundi, Lugalo jijini Dar es Salaam.

TDS ilianza kwa kutoa kipigo cha mabao 9-1 dhidi ya Kakakuona katika Kundi A, huku Bulls Football Academy iliyopo Kundi B ikiibamiza Brothers Jr mabao 3-0.

Ushindi mnono wa TDS ambayo ni timu maalum iliyoanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya programu ya utambuzi wa vipaji ulipambwa na kiwango bora cha mchezaji Abiud Richard Faru aliyetupia mabao matatu (hat-trick) na kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.

Katika mechi hiyo, TDS ilionekana kutawala zaidi mchezo kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho, ikitumia takribani asilimia 80 ya nafasi ilizokuwa inatengeneza.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa Kundi A uliopigwa, Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni, Kocha Mkuu wa TDS, Henry Sempa amesema siri ya mafanikio yao ilikuwa ni uwezo wa wachezaji wake kupora mipira katika nusu ya uwanja ya wapinzani wao na kutumia vyema mbinu walizofanyia kazi mazoezini.

“Tunaamini sana kwenye maendeleo ya wachezaji kwa kuwapa nafasi ya kucheza mechi za kiushindani. Wanapopata mashindano kama haya wanaongeza uzoefu zaidi na kukua. Pia tunatumia fursa hii kufanya scouting ya wachezaji ili kusaidia taifa,” amesema Sempa.

Mchezaji bora wa mechi hiyo, Abiud Richard Faru, alieleza furaha yake baada ya kufanya vizuri katika mechi yake ya kwanza ya mashindano hayo, akisema:

“Nashukuru kwa kufunga mabao matatu na kuibuka mchezaji bora. Wapinzani wetu walionyesha kiwango bora ingawa tulifanikiwa kuwazidi kimbinu. Najipanga kufanya vizuri zaidi mechi zijazo.”