Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashindano pickleball kufanyika mwezi ujao

PICK Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa michezo hiyo ni pamoja na Pickleball, mchezo unaozidi kupata umaarufu kutokana na urahisi wake, mvuto wake na uwezo wa kuwashirikisha watu wa rika mbalimbali, huku mashindano yake yakitarajiwa kufanyika mwezi ujao.

KATIKA ulimwengu wa michezo unaoendelea kubadilika kuna michezo inayokuja na upekee wa aina yake, ikichanganya burudani, afya, ushindani na fursa za kijamii.

Miongoni mwa michezo hiyo ni pamoja na Pickleball, mchezo unaozidi kupata umaarufu kutokana na urahisi wake, mvuto wake na uwezo wa kuwashirikisha watu wa rika mbalimbali, huku mashindano yake yakitarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Pickleball siyo mchezo wa raketi pekee; ni jukwaa la kujenga afya, kuimarisha mahusiano, kukuza vipaji na kuhamasisha jamii kuthamini umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa mchezaji au mtu anayeshiriki kucheza mchezo huo.

Nchini Tanzania, mchezo huu una fursa kubwa ya kukua na kujipatia nafasi katika tasnia ya michezo, hasa kupitia juhudi mbalimbali kutoka kwa wadau wanaoutambua umuhimu wake ambao wanaufanya mchezo huu kujua zaidi.

Miongoni mwa wadau hao ambao ni kioo cha mchezo huo huku wakitumia nguvu zao kuhakikisha Pickleball inakua nchini na inatambulika ni Dkt Sajad Habib Rai mchezaji na mfadhili wa mchezo huo. Dkt Sajad mzalendo ambaye amejitolea kuhakikisha Pickleball inakuwa nchini, anasema dhamira yake siku zote ni kuona vijana hasa wapenda michezo wanakuwa na uwanja mpana wa kuibua vipaji vyao kupitia fursa mbalimbali za michezo zinazojitokeza nchini.

BAL 02

Anasema kutokana na kuona uzuri wa mchezo huo na muamko wa baadhi ya vijana kuupenda mchezo huo akiwemo binti yake ambaye ndiye alimshawishi kuucheza mchezo huo na yeye kuona Kuna kila haja ya kuwainua vijana wengi ambao nao wamevutia kucheza Pickleball.

“Mimi ni mpenda michezo, tangu nikiwa mdogo nimeshiki michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu ambapo kwa hapa nchini nimewahi kuitwa hadi katika timu ya vijana, kwa Pickleball ni fursa ambayo nataka tuufanye kuwa moja ya mchezo mahili hapa nchini kwetu,” anasema Dkt Sajad

Anasema Tanzania Ina vipaji vikubwa vya michezo ikiwemo Pickleball zaidi kinachohitajika ni wadau mbalimbali kujitoa na kuwashika mkono ili Taifa liweze kuwa na wachezaji wakubwa wa kuliwakilisha katika michuani ya kimataifa.

Anasema pamoja na uwepo wa vipaji hivyo na changamoto wa vijana wengi kukosa watu wa kuwashika mkono ili waweze kupiga hatua, upungufu wa viwanja au maeneo ya kuchezea mchezo huo ni changamoto nyingine kubwa ambayo kama ikitatuliwa itaufanya mchezo huo kufika mbalimbali.

BAL 01

Dk Sajad anasema vipo baadhi ya viwanja ambavyo hapo awali vilikuwa vikitumika kuuchezea mchezo huo vimeingia katika migororo hali ambayo imesababisha changamoto kubwa kwa wachezaji wengi

Anasema endapo Serikali itaweka nguvu kuhakikisha migogoro iliyopo katika viwanja hivyo inatatuliwa sambamba na kuwashika mkono vijana wenye dhamira ya kucheza mchezo huo, anaamini kuwa ipo Tanzania itatawazwa mabingwa wa Dunia wa mchezo wa Pickleball.

Anasema kwa Sasa sifa kubwa ambayo Tanzania inayo katika mchezo huo ni pamoja na kupeleka timu ya Taifa ya mchezo huo katika fainali za Dunia zilizofanyika Agosti Mwaka huu nchini Vietnam huku waamuzi wake wawili wakifanikiwa kuchezesha fainali za mchezo huo.

Kwa upande wake mkufunzi wa mchezo huo  wa Pickleball, Abdallah Manyua anasema Tanzania inahitaji wadau wa kutosha wa kuifanya Pickleball kuwa mchezo wenye nguvu zaidi katika siku zijazo huku akisisitiza kuhusu suala la uwepo wa vipaji vingi vya mchezo huo.

Abdallah anasema mchezo wa Pickleball siyo tu kwamba unaonesha kuwa na vipaji vya kutosha hapa nchini, bali pia una wataalam wengi wanaofundisha hali inayochangia kupatikana kwa vipaji vipya kila siku huku akipigia chapuo kwa wadau kujitokeza na kuunga mkono hususani katika upatikanaji wa vifaa vya uchezaji.

Anasema wachezaji wa mchezo huo wapo wengi,  isipokuwa baadhi yao wanashindwa kumudu gharama ndogo za ununuzi wa vifaa vya uchezaji  zikiwemo ‘racket’ sambamba na malipo kwa wakufunzi wa mchezo huo. Anasema kimsingi Pickleball ni mchezo wa ‘raketi unaochanganya vipengele vya tenisi, tenisi ya mezani maarufu kama ping-pong na badminton. Huchezwa na wachezaji wawili, mmoja dhidi ya mwingine au wanne - wawili kila upande.

BALL Pict

 Unatumia raketi bapa na imara pamoja na mpira mwepesi wa plastiki wenye matundu, unaochezewa katika uwanja maalumu wenye wavu katikati. Uwanja wake una upana wa futi 20 na urefu wa futi 44, sawa na takribani mita 6.1 kwa mita 13.4.

Wavu una urefu wa takribani sentimita 91 kwenye kingo na sentimita 86 katikati ambapo muundo wake huufanya Pickleball kuwa mchezo wenye mchanganyiko wa kasi, mbinu, umakini na maamuzi ya haraka.

Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba mchezo huu hauhitaji uwanja mkubwa kama wa tenisi hali inayowafanya kuwa na uwezekano wa kuanzishwa katika shule, vyuo, vilabu, vituo vya burudani na maeneo mengine yanayofaa kwa shughuli za michezo.