Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAONI: Simba inahitaji utulivu mkubwa

UNAWEZA kusema hali sio shwari sana ndani ya klabu ya Simba na siyo tu baada ya kichapo walichopata kutoka kwa watani zao, Yanga waliowafungwa mabao 5-1 wikiendi iliyopita.

Hali ndani ya Simba si nzuri kwa muda mrefu ila ni kwa vile tu timu inapata matokeo mazuri kwenye mechi nyingi wanazocheza, hakuna kelel nyingi huku mitaani.

Simba inapata matokeo mazuri uwanjani ingawa mashabiki hawaridhiki na kiwango inachoonyesha lakini wanapozwa tu na mafanikio.

Lakini kinachosemwa ni kwamba Simba kuna matatizo makubwa ya kiuongozi ambayo ni anguko kwa timu ambalo hasa ndilo tunaliona.

Inawezekana  mashabiki wameiona timu ni mbovu baada ya kichapo hicho, lakini ukweli ni kwamba Simba haipo vizuri na kama ni wazuri basi ni kwa mchezaji mmoja mmoja jambo ambalo haliwezi kuisaidia.

Ukiangalia kwenye msimamo inashika nafasi ya pili lakini inashinda kibahati bahati na wakati mwingine huku mashabiki wake wakishika roho zao mikononi mpaka mechi inapomalizika. Kinachowauma na kuanza kuonekana zaidi kwamba mambo si shwari kwa mabosi wa klabu ni hiki kipigo, vinginevyo mambo yangeendelea kwenda kimyakimya.

Sasa ni kama kila kitu kipo wazi, tetesi ambazo zinaweza kuwa kweli ama uongo zinazungumzwa, hivyo maswali ni mengi kwa mashabiki lakini ndani ya viongozi hao hao nao hawajatulia kwani wanahaha kuona kwamba mambo yanatulia.

Mabosi wa Simba hawaishi kufanya vikao kuona ni namna gani upepo utatulia ili hata dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa wawe na utulivu wa akili kuongeza wachezaji wenye msaada kwao.

Simba si kwamba haijasajili, imesajili lakini usajili wao hauna faida yeyote zaidi ni wachezaji wawili hasa wa kigeni ndiyo wameonyesha ubora wao Fabrice Ngoma na Che Malone, wengine bado mwendo ni mdogo mdogo tofauti na wengi waliotarajia.

Mambo ambayo viongozi wa Simba wanapaswa kuhaha nayo ukiachana na tofauti zao wenyewe ni kuwapa furaha mashabiki na wanachama wao ambao ndiyo wenye timu kuongeza umakini katika maboresho ya kikosi chao.

Kikosi cha Simba ukikiangalia nguvu wanayoitumia sasa ni ile ya msimu uliopita kwa wachezaji ambao ni wale wale wanaoipambania timu miaka yote, jambo ambalo wengi wanajiuliza kwanini viongozi wa Simba wanashindwa kufanya maamuzi ya kusajili wachezaji mbadala.

Inawezekana kuna mbadala ambao wao wanaona wamesajili lakini kazi yao ni ipi kwani wapo kama watumishi hewa ndani ya kikosi, hawaaminiki kabisa wakati wao ndio waliwasajili wakiamini kabisa katika viwango vyao. Timu imejaa mafaza ambao wana uamuzi na nguvu ya kuamuru nini wanataka.

Kwa Simba hii ambayo imeondoka kwenye mfumo wa kizamani haipaswi kukumbatia hayo. Inatakiwa kuwa na wachezaji wanaojua na kutambua majukumu na sio kuleta urafiki. Simba ijitathimini kwani ina jukumu kubwa mbele, ligi inaendelea na inakwenda kucheza mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kujivuruga kwao na kukosa utulivu kunaweza kuwaharibia huko mbele.