Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makapu ashonwa nyuzi tatu Mbuni FC

MAKAPU Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyetamba na timu mbalimbali za Yanga, Ihefu kwa sasa Singida Black Stars, Mashujaa FC, Geita Gold na Bigman FC, amesema anaamini uzoefu wake katika kikosi hicho cha Mbuni FC, utaleta mabadiliko chanya, licha ya ushindani uliopo.

KIUNGO mkabaji wa Mbuni FC ya jijini, Arusha, Said Juma ‘Makapu’ ameshonwa nyuzi tatu juu ya paji lake la uso, baada ya kugongana na mchezaji wa Gunners FC ya Dodoma, Issa Kinjumbi katika mechi ya Championship, iliyopigwa, Oktoba 2, 2026.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh, Amri, Abeid, jijini, Arusha na Mbuni kushinda mabao 2-0, Makapu aligongana na Issa dakika ya 70, jambo lililosababisha kushindwa kuendelea kucheza kisha kukimbizwa haraka hospitalini.

Akizungumza na Mwanaspoti, Makapu amesema baada ya tukio hilo alikimbizwa hospitalini na kupatiwa msaada wa haraka wa kushonwa nyuzi tatu katika paji lake la uso kutokana na kadhia aliyoipata, japo kwa sasa anaendelea vizuri na matibabu. “Nimepewa wiki moja hadi mbili za uangalizi zaidi baada ya kushonwa nyuzi tatu, nashukuru jopo la madaktari kwa msaada wa haraka walionipatia, lengo langu ni kurudi ili kuendelea kuipigania timu ifanye vizuri msimu huu,” amesema Makapu.

Nyota huyo aliyetamba na timu mbalimbali za Yanga, Ihefu kwa sasa Singida Black Stars, Mashujaa FC, Geita Gold na Bigman FC, amesema anaamini uzoefu wake katika kikosi hicho cha Mbuni FC, utaleta mabadiliko chanya, licha ya ushindani uliopo.