Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makapu aanza tambo Mbuni FC

MAKAPU Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Makapu amesema mechi tano za mwanzo zilikuwa ngumu kwa kikosi hicho, lakini kwa sasa kuna maendeleo katika uchezaji na maelewano baina ya wachezaji, jambo linalowapa ari ya kuendelea kupambana ili kumaliza msimu katika nafasi nne za juu.

KIUNGO mkabaji wa Mbuni FC ya jijini Arusha, Said Juma ‘Makapu’, amesema timu hiyo imeanza kurejea kwenye kiwango chake baada ya mwanzo mgumu wa msimu wa 2026/27, hali inayoongeza matumaini ya kupanda kwenye msimamo wa Ligi ya Championship.

Akizungumza na Mwanaspoti, Makapu amesema mechi tano za mwanzo zilikuwa ngumu kwa kikosi hicho, lakini kwa sasa kuna maendeleo katika uchezaji na maelewano baina ya wachezaji, jambo linalowapa ari ya kuendelea kupambana ili kumaliza msimu katika nafasi nne za juu.

“Mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu wachezaji wengi tulikuwa bado hatujaelewana kuhusu aina ya uchezaji wetu kutokana na ugeni. Lakini kwa sasa tumeanza kujipata vizuri na kuongeza ushindani tofauti na tulivyoanza msimu wa 2026/27,” amesema Makapu.

Kiungo huyo, aliyewahi kuzitumikia timu mbalimbali zikiwemo Yanga, Ihefu, Singida Black Stars, Mashujaa FC, Geita Gold na Bigman FC, amesema anaamini uzoefu wake ndani ya kikosi cha Mbuni FC utasaidia kuleta mabadiliko chanya, licha ya ushindani uliopo.

Kabla ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya TMA FC ya Iringa, Mbuni FC ilikuwa imecheza mechi 11, ikishinda nne, kutoka sare tatu na kupoteza nne, ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo kwa pointi 15.

Katika mechi hizo, safu yake ya ushambuliaji ilikuwa imefunga mabao 15, huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao 17.