Majina ya mastaa Simba, Yanga yapigwa chini

WAFANYABIASHA wameeleza kuacha kuandika majina ya mastaa wa soka nchini kutokana na kutotulia kwenye timu kwa muda mrefu hivyo wao kupata hasara katika mauzo.

Majina ya mastaa ambayo hupenda kuandikwa kwenye jezi ni wale wa timu za Simba na Yanga zaidi.

Imeelezwa kwamba hasara wanayoipata ni pale ambapo mastaa hao wanapoachana na timu hizo hivyo mashabiki wa timu aliyokuwa hawawezi kununua tena jezi ya mchezaji huyo, inawalazimu watengeneze jezi ya timu aliyohamia kitu ambacho sasa hivi hawakitaki.

Mfanyabishara wa jezi hizo maarufu kwa jina la Zimala wa Zimala ambaye makazi yake ni jijini Dar es Salaam alisema kuwa miaka ya hivi karibuni walikuwa wanauza jezi zilizochapishwa majina ya mastaa mgongoni na waliuzwa kwa asilimia kubwa tofauti na sasa.

Alisema kuwa wachezaji kutokuw ana msimamo na maisha yao ya soka kunayumbisha soko lao ndio maana wameamua kuacha kuchapisha majina yao ili kulinda soko lao.

"Mauzo kwa ujumla ni nusu kwa nusu ingawa jezi za Yanga hazitoki kwa haraka kiivyo kama ilivyo Simba, hii ni kwasababu Simba wametambua hata watu wa hali ya chini hivyo unaweza kuuza jezi zao hata Sh 10000 tofauti na Yanga imekomea Sh 35000.

"Tumeacha kuandika majina ya mastaa kwasababu hawatabiriki kwenye usajili yaani hawatulii na timu moja kwa muda mrefu, hivyo unaweza andika jina msimu huu yupo simba lakini kabla hata msimu haujaisha anahama unazimika kuandika tena wakati zile za kwanza hazijaisha.

"Hii ilikuwa inatuingizia hasara kubwa maana mchezaji akihama hakuna atakayenunua jezi yake, lakini kwa ufupi biashara ya hapa na Bara hakuna tofauti," alisema Zimala