Tiketi Simba, Yanga zauzwa kama njugu

Wednesday January 13 2021
tiketi pic
By Mwanahiba Richard

UNGUJA. TIKETI za kuingia kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi  inayowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga zimeonekana kugombewa huku tiketi za VIP zinazouzwa Sh 15,000 zikiwa zimeisha.

Tiketi hizo huuzwa kwa bei ya sh 5000, 10000 na 15000 baada ya kuwepo mabadiliko ambapo awali ziliuzwa Sh 3000, 5000 na 10000.

Idadi ya tiketi zilizotangazwa kuuzwa ni 12000 ambayo ni idadi ya mashabiki wanaoingia uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Mashabiki walionekana kutafuta tiketi hizo ambapo Mwanaspoti Online ilijiridhisha kwamba kweli tiketi za VIP zimemalizika mapema kutokana na watu wengi kujitokeza kununua huku mpaka saa 4 asubuhi zilibaki tiketi za Sh 5000 na 10000 ambazo pia zilinunuliwa kwa wingi.

Jana Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Khamis Said alisema hakutakuwepo na ongezeko la tiketi hivyo shabiki atakayekosa atalazimika kuangalia akiwa nyumbani.

"Hatuwezi kuongeza uchapaji wa tiketi kwa sababu uwanja hauna uwezo wa kubeba watu wengi, hivyo shabiki atakayekosa atalazimika kuangalia akiwa nyumbani.

Advertisement

"Hatuwezi kuongeza uchapaji wa tiketi kwa sababu uwanja hauna uwezo wa kubeba watu wengi, hivyo mashabiki tulipa taarifa mapema juu ya hilo," alisema Said

Advertisement