Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Machupa asimulia moto wa Mpanzu ulivyomtesa

Mbeya. Licha ya Fountain Gate kupoteza kwa bao 1-0, kipa Machupa Juma alionyesha uwezo mkubwa wa kuzuia hatari alizoelekezewa na washambuliaji wa Simba.

Katika mahojiano yake na Spoti Mikiki, Machupa amesimulia mchezo huo pamoja na historia ya maisha yake kisoka.


Historia yake

Kipa huyo mzaliwa wa mkoa wa Mara, aliibukia katika Kituo cha Mara Sports ambacho kilimtambulisha hadi mwaka 2021 alipojiunga na Fountain Gate.

Alifanya vizuri hadi mwaka jana alipopandishwa katika kkosi cha wakubwa akicheza mechi 15.


Atoa matumaini

Licha ya kukiri ugumu wa ligi na hali ya matokeo waliyonayo kwa sasa Fountain Gate, Machupa anasema wameanza na upepo mbaya akieleza kuwa bado hawajakata tamaa na matarajio yao ni kufanya vizuri.

Anaeleza kuwa mechi 10 walizocheza na kuvuna pointi sita si matokeo mazuri sana kwa timu yenye mipango na malengo akieleza kuwa kwa sasa wanasaka japo mechi tatu tu za kushinda ili kubadili upepo.

“Matokeo si mazuri na inatupa presha lakini hatujakata tamaa kwa kuwa bado ligi haijaisha na ndio kama imeanza. Tunasaka michezo mitatu ya ushindi ya kuturejesha kwenye mstari.

“Matarajio yangu ni kwamba kila mmoja akipambana kwa uwezo na juhudi zake tunaweza kusahihisha makosa na kujiweka pazuri. Kwa sasa kila mechi ni vita ya pointi tatu,” amesema kipa huyo.


Mpanzu ni moto

Machupa anasema katika mchezo dhidi ya Simba pamoja na matokeo ya jumla, lakini hawezi kumsahau Elie Mpanzu ambaye alikuwa moto muda wote na alimtesa sana.

“Mpanzu alikuwa mwiba sana ndiye alinitesa sana japokuwa nashukuru nilionesha uwezo na juhudi zangu binafsi kudhibiti hatari zote. Hakunipa utulivu na muda wote alinishambulia ila nashukuru tulikuwa imara uwanjani

“Tulijua Simba ni timu kubwa na ina wachezaji bora Afrika, hivyo kilichofanyika ni kupambana nao kila mmoja kuwania pointi tatu,” anasema Machupa.


Ndoto zake

Kinda huyo anasema kuwa ndoto zake ni kuona anafikia malengo ya kuzitumikia timu kubwa nchini Simba na Yanga.

“Malengo yangu ni kufika mbali kwa kuwa naamini ukicheza moja ya timu hizo (Yanga, Simba na Azam) unapata nafasi kubwa ya kuonekana hadi Afrika. Naamini kwa kuwa bado mdogo naweza kutimiza ndoto hiyo,” anasema Machupa.

Anasema hadi sasa anaendelea kujipambania katika kikosi cha Fountain Gate akikiri ugumu wa namba na jinsi anavyomshawishi kocha Fred Felix ‘Minziro’ kuendelea kumuamini kuanzia mazoezini hadi mechi.

“Mazingira ni mazuri kwa ujumla japokuwa kila mmoja huwa anatamani kupata changamoto mpya, kujituma na kuonesha kitu cha ziada uwanjani vitu ambavyo anaamini vitamhakikishia namba kikosini,” anasema.


Hamasa iko hapa

Kipa huyo anasema licha ya kuupenda mpira tangu akiwa mdogo lakini alikuwa akivutiwa na Kipa wa zamani wa Simba, Aisha Manula (kwa sasa Azam) na alikuwa sehemu ya hamasa kwake.

“Mimi nilikuwa beki wa kati ila miaka hiyo nikawa namuangalia sana Manula nikaona ananivutia uchezaji wake nikaamua kubadili nafasi kuingia golini hadi sasa” anasema Machupa.