Mabula ataka kuonyesha alichokifanya Taifa Stars
Muktasari:
- Kabla ya hapo, msimu wa 2024/25 akiwa Shamakhi, kiungo huyo alicheza mechi 17, akifunga mabao matatu na kutoa asisti moja. Takwimu hizo zinaonyesha mchango wake katika safu ya kiungo.
KIUNGO wa JS Kabylie ya Algeria, Alphonce Mabula amesema anatamani kuendeleza ari aliyoionyesha akiwa na Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu Afcon 2027.
Mabula amesema anataka kuendelea kuonyesha kiwango kizuri katika klabu hiyo mpya, akiamini mwendelezo wa kiwango alichokionyesha akiwa na timu ya taifa unaweza kumsaidia kukabiliana na ushindani wa Ligi Kuu ya Algeria.
Akizungumza kuhusu majukumu yake, kiungo huyo amesema: “Kazi yangu ni kucheza mpira, hivyo nikiwa kwenye ligi ngumu kama ya Algeria na nikapata nafasi ya kucheza mara kwa mara, inaniongezea kujiamini zaidi.”
Ameongeza anataka kutumia nafasi atakazopata kuonyesha uwezo wake na kusaidia timu yake kufanya vizuri.
Mabula anakipiga kwenye ligi hiyo baada ya kujiunga nayo msimu huu akitokea Shamakhi FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Azerbaijan. Katika msimu wa 2025/26, alicheza mechi 32 za mashindano yote, akifunga mabao matatu.
Kabla ya hapo, msimu wa 2024/25 akiwa Shamakhi, kiungo huyo alicheza mechi 17, akifunga mabao matatu na kutoa asisti moja. Takwimu hizo zinaonyesha mchango wake katika safu ya kiungo.