Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars yaanza kwa kichapo nyumbani AFCON 2027

AFCON Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo wa Kundi L uliochezwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, wageni Guinea-Bissau walipata bao la kwanza dakika ya 33, mfungaji akiwa Franculino Djú aliyeachia shuti kali nje ya boksi na kumshinda kipa wa Taifa Stars, Zuber Foba. Bao hilo lilitokana na mabeki wa Taifa Stars, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca kushindwa kuokoa hatari wakati mpira alipokuwa nao Norberto Betuncal ‘Beto’, aliyetoa pasi kwa mfungaji aliyekuwa mwenyewe bila kukabwa.

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) baada ya kufungwa nyumbani kwa mabao 2-0 na Guinea-Bissau.

Mchezo huo wa Kundi L uliochezwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, wageni Guinea-Bissau walipata bao la kwanza dakika ya 33, mfungaji akiwa Franculino Djú aliyeachia shuti kali nje ya boksi na kumshinda kipa wa Taifa Stars, Zuber Foba. Bao hilo lilitokana na mabeki wa Taifa Stars, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca kushindwa kuokoa hatari wakati mpira alipokuwa nao Norberto Betuncal ‘Beto’, aliyetoa pasi kwa mfungaji aliyekuwa mwenyewe bila kukabwa.

Kabla ya bao, dakika ya 14, mshambuliaji wa Taifa Stars, Charles M’mombwa alimpasia Simon Msuva akiwa karibu na goli la Guinea Bissau, lakini shuti lake lilipaa juu na kushindwa kuipa bao la uongozi.

Mashambulizi ya hapa na pale kipindi cha kwanza, yalikuwa na faida kubwa kwa Guinea-Bissau ambao walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

AFCO 01

Kipindi cha pili kilikuja tofauti ambapo dakika ya 55, Guinea-Bissau ilifanya mabadiliko, akitolewa Iano Simão na kuingia Adramane Cassama. Mabadiliko hayo ni kama yaliongeza nguvu kwa Guinea-Bissau kwani dakika ya 58, nahodha Mama Balde aliongeza bao la pili akimalizia pasi ya Euciodálcio Gomes.

Dakika ya 62, Kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi naye alifanya mabadiliko, aliwatoa Himid Mao, Charles M’mombwa na Seleman Mwalimu, wakaingia Mudathir Yahya, Alphonce Mabula na Tarryn Allarakhia

Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuwa na faida kwani hadi dakika ya mwisho, mwamuzi wa kati kutoka Zimbabwe, Brighton Chimene anapuliza filimbi, Taifa Stars ililala kwa mabao 2-0. Baada ya mchezo huo, Septemba 29, 2026, Taifa Stars itakwenda Morocco kucheza mechi yake ya pili dhidi ya Madagascar watakaokuwa mwenyeji. Katika Kundi L, mbali na Tanzania ambayo tayari ina tiketi ya AFCON 2027 kutokana na kuwa moja ya taifa mwenyeji, pia zipo Guinea-Bissau, Madagascar na Nigeria. Fainali za AFCON 2027 zitachezwa kuanzia Juni 19, 2026 hadi Julai 19, 2026 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.