Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula afurahi kuichapa USM Alger

MABULA Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo wa mabao 2-0 umeiwezesha JS Kabylie kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Algeria ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa, ikishinda sita, kutoka sare mbili na kupoteza moja.

KIUNGO wa Tanzania, Alphonce Mabula amesema ushindi wa mabao 2-0 walioupata JS Kabylie dhidi ya USM Alger katika mchezo wa Ligi Kuu ya Algeria ni matokeo makubwa kwao, hasa kutokana na umuhimu wa mchezo huo katika mbio za kuwania nafasi ya kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mabula amesema waliingia kwenye mchezo huo wakifahamu kuwa ushindi ungewawezesha kupanda hadi kileleni mwa msimamo, hivyo matokeo hayo yamewapa furaha na kuongeza morali ndani ya kikosi.

“Hii ni kitu kikubwa sana kwetu, maana ilikuwa mechi muhimu. Tulihitaji kushinda ili tukae kileleni,” amesema Mabula, akieleza umuhimu wa matokeo hayo kwa timu yake.

Amesema hawakupata ushindi huo dhidi ya timu nyepesi, akisisitiza kuwa USM Alger ni wapinzani wenye ubora na uzoefu, jambo lililoufanya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa.

MABU 05

“Na USMA ni timu nzuri, ukizingatia wametoka kumpiga Mamelodi Sundowns kwenye Super Cup. Kwa hiyo wana timu nzuri. Ilikuwa mechi nzuri na tumepata matokeo mazuri,” amesema kiungo huyo.

Ushindi huo wa mabao 2-0 umeiwezesha JS Kabylie kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Algeria ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa, ikishinda sita, kutoka sare mbili na kupoteza moja.