Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabeki wamliza kocha Uhamiaji

MABEKi Pict

Muktasari:

  • Oktoba 4, 2026, Uhamiaji ilipoteza mechi hiyo ya Ligi Kuu Zanzibar kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa JKU kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

WAKATI Uhamiaji ikifungwa kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Zanzibar, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sheha Khamis mesema safu ya beki ilifanya makosa yaliyochangia kipigo hicho.

Oktoba 4, 2026, Uhamiaji ilipoteza mechi hiyo ya Ligi Kuu Zanzibar kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa JKU kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Kocha Sheha amesema hawakupaswa kufungwa kwa namna ambavyo timu ilicheza na mipango lakini mabeki walishindwa kufuata maelekezo yake hasa kipindi cha kwanza na hatimaye kupoteza.

“Safu ya beki ilifanya makosa ambayo wapinzani walichukulia kuwa faida kwao na kutuadhibu, licha ya kutengeneza nafasi nyingi kuliko JKU, bahati haikuwa kwetu, tukapoteza,” amesema.

Amesema baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo watayafanyia kazi kuhakikisha hayajirudii katika mechi inayofuata dhidi ya Mafunzo itakaochezwa Oktoba 10, 2026.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Uhamiaji imeendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sita, ikishinda tano.