Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yatibua mipango ya Uhamiaji

Muktasari:

  • Kabla ya mchezo huo, Uhamiaji ilikuwa miongoni mwa timu tatu ambazo hazijapoteza mchezo wowote katika ligi hiyo, nyingine zikiwa Zimamoto na Polisi.

JKU imeivuruga mipango ya Uhamiaji baada ya kuichapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) uliopigwa Oktoba 4 mwaka huu.

Kabla ya mchezo huo, Uhamiaji ilikuwa miongoni mwa timu tatu ambazo hazijapoteza mchezo wowote katika ligi hiyo, nyingine zikiwa Zimamoto na Polisi.

Hata hivyo, kichapo hicho kimeifanya Uhamiaji kupoteza mchezo wake wa kwanza katika mechi sita, na kuendelea kubaki nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na pointi 15.

Ushindi huo umeiwezesha JKU kuishusha KVZ na kupanda hadi nafasi ya nne, huku pia ukivuruga hesabu za Uhamiaji iliyokuwa ikilenga pointi tatu ili kuipiku Zimamoto na kukaa kileleni. JKU ilianza mchezo kwa kasi na kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Ahmed Ali dakika ya 24 na Erick Deogratus dakika ya 36. Kipindi cha pili, Uhamiaji ilirejea ikiwa na nguvu zaidi na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 54 kupitia Seif Abdalla. Hata hivyo, JKU haikuruhusu wapinzani wake kurejea mchezoni, kwani ilifunga bao la tatu dakika ya 90+3 kupitia Bernald Thomas na kuhitimisha ushindi wa mabao 3-1. Matokeo hayo yameifanya Zimamoto kuendelea kuongoza msimamo ikiwa na pointi 16, moja zaidi ya Uhamiaji yenye pointi 15, huku Polisi ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 12. Uhamiaji itarejea uwanjani Oktoba 11 kuikabili Mafunzo kwenye Uwanja wa Mao A, wakati JKU itakuwa mwenyeji wa Blacksailors Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Pangatupu, Kaskazini Unguja.