Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabeki waigharimu JKU, yaambulia sare

JKU Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyowakutanisha wababe wawili wa ligi hiyo ambao msimu uliopita walimaliza nafasi mbili za juu kwenye msimamo, ilionekana kuwa na ushindani mkubwa huku mabingwa watetezi, KVZ wakipambana kuhakikisha wanafanya vizuri, lakini hakuna aliyefanikiwa kuondoka na ushindi.

KOCHA wa JKU, AbdulSaleh Mohammed, amesema sare ya bao 1-1 waliyoipata dhidi ya KVZ katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyochezwa juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Mao A kisiwani Unguja, imetokana na safu yake ya ulinzi kufanya uzembe.

Mechi hiyo iliyowakutanisha wababe wawili wa ligi hiyo ambao msimu uliopita walimaliza nafasi mbili za juu kwenye msimamo, ilionekana kuwa na ushindani mkubwa huku mabingwa watetezi, KVZ wakipambana kuhakikisha wanafanya vizuri, lakini hakuna aliyefanikiwa kuondoka na ushindi.

JKU iliyoanza kwa kasi na nguvu ya kutafuta uongozi, ilifanikiwa kupata bao lililofungwa na Luis Antony, ndipo Yakoub Said ‘Kenny’ akaisawazishia KVZ na kufanya hadi mwisho matokeo kuwa sare.

JK 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa JKU, AbdulSaleh Mohammed, amesema uzembe wa mabeki ndio ambao uliwagharimu na wapinzani kutumia kama faida upande wao.

Amesema JKU ilipaswa kushinda mechi hiyo kwa sababu walikuwa vizuri dhidi ya wapinzani wao kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo wachezaji wake walishindwa kuzitumia vizuri, huku kosa moja la safu ya ulinzi ndilo limewagharimu.

“Tulizipata nafasi nyingi lakini wachezaji wakifika katika eneo la kufunga wanashindwa kuzitumia vizuri,” amesema.

JK 02

Sare hiyo imeifanya JKU kukusanya pointi nane ikicheza mechi nne, wakati KVZ iliyocheza mechi mbili, ina pointi moja.

Mechi inayofuata JKU itashuka dimbani Septemba 30, 2026 kucheza dhidi ya KMKM kwenye Uwanja wa Pangatupu, huku KVZ ikichuana na Raskazone, Septemba 20, 2026 Uwanja wa Kitogani.