Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabao mawili, asisti moja, Davids atoa ujumbe Singida

Muktasari:

  • Davids alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja katika mechi mbili dhidi ya Al-Ghazal ya Sudan Kusini, ambazo Singida ilishinda kwa jumla ya mabao 10-1. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Juba, Singida ilishinda mabao 7-1 kabla ya kushinda 3-0 katika mechi ya marudiano.

WINGA wa Singida Black Stars, Henry Davids amesema kuanza vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika kumempa motisha ya kuendelea kupigania nafasi ndani ya kikosi hicho.

Davids alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja katika mechi mbili dhidi ya Al-Ghazal ya Sudan Kusini, ambazo Singida ilishinda kwa jumla ya mabao 10-1. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Juba, Singida ilishinda mabao 7-1 kabla ya kushinda 3-0 katika mechi ya marudiano.

Davids alisema kiwango hicho kimempa morali ya kuongeza juhudi kila anapopewa nafasi na kocha, akiamini ushindani mkubwa uliopo ndani ya kikosi unamlazimisha kila mchezaji kuonyesha kiwango bora.

“Kwangu ni mwanzo mzuri. Kufunga mabao mawili na kutoa asisti moja katika mechi mbili ni kitu kinachonipa motisha ya kuendelea kufanya kazi zaidi,” alisema Davids.

Alisema Singida Black Stars ina kikosi chenye wachezaji wengi wenye uwezo, hivyo kupata nafasi ya kucheza si jambo rahisi, lakini amedhamiria kutumia kila nafasi anayopewa kuonyesha uwezo wake.

“Ushindani ni mkubwa kwa sababu tuna wachezaji wengi wazuri. Mimi nikipewa nafasi yangu ni kuhakikisha naitumia vizuri. Hiyo ndiyo sehemu yangu ya kuonyesha ubora wangu na kumfanya kocha azidi kuniamini,” alisema.

Winga huyo alijiunga na Singida msimu huu akitokea Fountain Gate, ambako alicheza mechi 21 na kufunga mabao manne.