Mkude afunguka kuibeba Mashujaa
Muktasari:
- Msimu uliopita Mkude alikuwa nje ya kazi baada ya kuachana na Yanga, aliyoichezea kuanzia 2023 hadi 2025. Amesema kinachobadilika sasa ni timu, lakini majukumu yake uwanjani yanaendelea kuwa yale yale.
KIUNGO mkabaji wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Jonas Mkude amesema kujiunga na Mashujaa ni nafasi ya kuendelea na majukumu yake katika soka, huku akisisitiza kikubwa kwake ni kuha kikisha huduma yake ina kuwa msa ada kwa timu hiyo.
Msimu uliopita Mkude alikuwa nje ya kazi baada ya kuachana na Yanga, aliyoichezea kuanzia 2023 hadi 2025. Amesema kinachobadilika sasa ni timu, lakini majukumu yake uwanjani yanaendelea kuwa yale yale.
“Kitu kikubwa ni kufanya kazi itakayoon yesha uw epo wangu katika timu ya Mashujaa, kama ambavyo ilikuwa katika timu nyingine nilizoc hezea kwa misimu tofauti,” alisema Mkude.
“Ni msimu mgumu, lakini kama mchezaji nachukulia kama changamoto ya kuonyesha kiwango cha kuisaidia timu ili iweze kufikia malengo yaliyopangwa na viongozi.”
Mkude, ambaye kwa muda mrefu alidumu Simba baada ya kupandishwa kutoka kikosi B msimu wa 2011-2012 hadi 2023 kabla ya kujiunga na Yanga, amesema ana furaha ya kuanza ukurasa mpya akiwa Mashujaa.
“Najisikia furaha kuwepo Mashujaa. Kila kitu kinapangwa na Mungu, ingawa katika mpira wa miguu sidhani kama kuna jambo jipya zaidi ya kupambana,” alisema.
Akiwa Simba Mkude alitwaa medali za ubingwa wa Ligi Kuu katika misimu ya 2011-2012, 2017-2018, 2018-2019, 2019-2020 na 2020-2021, kabla ya kuongeza nyingine mbili akiwa Yanga msimu wa 2023-2024 na 2024-2025.
Kiungo huyo baada ya kutua Mashujaa msimu huu, Septemba 9, 2026 alicheza mechi yake ya kwanza Ligi Kuu Bara kwa dakika nane akiingia kutokea benchi.
Kwa sasa Mashujaa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi tisa katika mechi sita ilizocheza.