Maandalizi ya AFCON kufikia ukomo Desemba 2026
SERIKALI ya Tanzania imejihakikishia hadi Desemba 2026, maandalizi yote ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, yatakuwa yamefikia ukomo kwa zaidi ya aslimia 90, hadi 100.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema licha ya ukaguzi wa mara kwa mara kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), ila malengo ya Serikali ni kufikia ukomo Desemba 2026.
"Tunashukuru CAF kwa kuendelea kuonyesha imani kubwa kwetu katika maandalizi ya AFCON mwakani, sisi kama Serikali tunataka hadi kufikia Desemba 2026, tumekamilisha kila kitu," amesema Makonda.
Aidha, Makonda amesema viwanja vingi vitakavyotumika kwa maana ya mazoezi na kuchezea viko katika hatua nzuri, jambo linaloonyesha matumaini makubwa kwa taifa letu, wakati wa mashindano hayo mwakani.