Libolo na timu ya Okwi zapeta CAF
MWANDISHI WETU ETOILE du Sahel ya Tunisia anayoichezea Emmanuel Okwi imeshinda mabao 2-1 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho huku Recreativo Libolo ikishinda idadi hiyo hiyo ya mabao nyumbani dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Okwi alijiunga na Etoile akitokea Simba na amesajiliwa kwenye mashindano hayo, lakini bado hajaanza kutumika kikamilifu kwani aliingizwa dakika ya 72 katika mechi hiyo mwishoni mwa wiki. Mabao yao yalifungwa na Mossaab Sassi na Rami Bedoui ambao wote ni wazawa. Kwa upande wa Libolo ambayo iliitoa Simba ya Tanzania kwenye hatua ya mtoano, wikiendi iliyopita iliichapa El Merreikh ya Sudan mabao 2-1 na kama ikifanikiwa kushinda mchezo ujao ugenini itacheza na mshindi kati ya Enugu Rangers ya Nigeria na Vital'o ya Burundi.