Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Morrison, Djuma walisimamishwa Yanga

MASTAA watatu wa Yanga, wameonja joto la jiwe baada ya kusimamishwa na kocha Nasreddine Nabi kutokana na utovu wa nidhamu.
Mastaa hao ni Djuma Shaban, Farid Mussa na Benard Morrison ambao wamekosekana kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara, kutokana na utovu wa nidhamu.
BM33, Shaban Djuma na Farid Mussa ndio wachezaji ambao waliondolewa kikosini kutokana na kuchelewa kuripoti kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili.

Wakati Farid na Djuma wakirejea kwenye kikosi hicho, Morrison amepelekwa kwenye kamati ya maadili ya klabu hiyo kwa ajili ya utovu wa nidhamu.
Mastaa wote wa Yanga, walipewa mapumziko hayo baada ya kumaliza mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kililiambia Mwanaspoti, wachezaji hao walishindwa kuripoti kambini siku iliyokuwa inatakiwa siku iliyofuata waliporudi kocha Nabi aliwatimua.
"Wachezaji hao walizingua na kocha Nabi akawapa adhabu ya kimya kimya, ila tayari wameshaomba radhi na kurejeshwa kikosi na wameingia kambini na wenzao tayari kwa mchezo ujao dhidi ya Prisonms," kimesema chanzo hicho kutoka ndani ya Yanga.
Wachezaji hao walizikosa mechi tatu za ligi dhidi ya Dodoma Jiji, Ihefu FC na Mbeya City ambapo Yanga ikishinda mbili na kupoteza mbele ya Ihefu na kukwamisha rekodi yao ya unbeaten iliyodumu kwa michezo 49 na kesho itashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Tanzania Prisons.