Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Nsingizini ajipa matumaini kupindua meza Kwa Mkapa

NSINGIZINI Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa nyota wa timu hiyo, Khanyakwezwe Shabalala, amekiri deni kubwa wanalokabiliana nalo kama wachezaji, ingawa sio kigezo cha kucheza kwa presha zaidi wakiwa ugenini.

KOCHA Mkuu wa Nsingizini Hotspurs, Mandla Qhogi, amesema licha ya kikosi hicho kupoteza kwa mabao 3-0, dhidi ya Simba katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, ila wana nafasi ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mandla, amesema anatambua ugumu uliopo wa kushinda ugenini kwa zaidi ya mabao manne, ingawa katika mpira wa miguu kila kitu kinawezekana pia.

INS 03

"Kabla ya mechi yetu ya kwanza hakuna aliyetarajia pia kama Simba ingeshinda ugenini kwa idadi kubwa ya mabao, hii ni mechi nyingine ngumu ila tutapambana kadri ya uwezo wetu."

INS 01

Aidha, Mandla amesema licha ya ugumu wa kupindua matokeo ya kwanza, ila watapambana kwa ajili ya Taifa lao na mashabiki wa Eswatini.

"Unapotaja miongoni mwa timu tano Barani Afrika huwezi kuiacha kuitaja Simba, tunatambua tunaenda kucheza kwenye uwanja wenye uwezo mkubwa wa kubeba mashabiki zaidi ya 60,000, hivyo, tuna kazi pia ngumu ya kufanya, ili tusonge hatua inayofuata."

Kwa upande wa nyota wa timu hiyo, Khanyakwezwe Shabalala, amekiri deni kubwa wanalokabiliana nalo kama wachezaji, ingawa sio kigezo cha kucheza kwa presha zaidi wakiwa ugenini.

INS 02

"Tumefanyia kazi mapungufu makubwa ambayo tulionyesha mechi yetu ya kwanza, hususani kuwaruhusu wapinzani wetu kutushambulia kwa kutushtukiza," amesema Shabalala.