Kocha Mlandege aipigia hesabu KMKM
Muktasari:
- Katika michezo minne ya mwisho timu ya Mlandege ilipoteza mitatu na kutoka sare mchezo mmoja hivyo ushindi huo wa pili tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2026-2027 baada ya kuifunga Muembe Makumbi bao 1-0.
KOCHA Msaidizi wa timu ya Mlandege, Sabri China amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kipanga umerudisha motisha na kujiamini kwa wachezaji hivyo anaahidi kuichakaza KMKM.
Katika michezo minne ya mwisho timu ya Mlandege ilipoteza mitatu na kutoka sare mchezo mmoja hivyo ushindi huo wa pili tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2026-2027 baada ya kuifunga Muembe Makumbi bao 1-0.
Sabri alisema, kupoteza michezo mitatu mfululizo iliwafanya baadhi wachezaji kutojiamini lakini tangu wameshinda mchezo hup mambo yamebadilika.
Alisema, wachezaji wengi wamebadilika na wanafanya vizuri katika uwanja wa mazoezi hali inayowapa moyo na matumaini ya kuwa bora mchezo unaofuata.
"Hali hii inanipa moyo kushinda mchezo unaofuata dhidi ya KMKM, tunajua ni mchezo mgumu kwa sababu hivi karibuni wapinzani wetu wanafanya vizuri lakini naamini tutashinda," alisema
China alisema, bado wana nafasi ya kuwa imara na bora Ligi Kuu Zanzibar kwani mechi zimebaki nyingi la muhimu washinde michezo iliyobakia.
Alisema kwa sasa ni ngumu kusema timu gani ina nafasi ya kuchukua ubingwa au ni timu zipi zitashuka daraja kwa sababu timu zimeachana alama chache sana.
Mlandege itashuka dimbani na KMKM Oktoba 18, 2026 katika uwanja wa Mao A, uliopo Unguja.